Na Mwandishi Maalum

Mkutano unaotathimini mafanikio ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa Miaka 10 kuhusu Nchi ambazo zipo nyuma kimaendeleo, ( Istanbul Program of Action for LDCs) unaendelea huko Antalya, Uturuki, ambapo imeelezwa kwamba nchi hizo 48 zilizomo katika kundi hilo bado zina safari ndefu.

Baadhi ya mambo yanayochelewesha mataifa hayo ku-graduate ambayo 38 ni kutoka Bara la Afrika, 13 kutoka Bara la Asia na moja kutoka Amerika ya Latini,ni pamoja na, umaskini uliokidhiri ambapo asilimia 51 ya idadi ya watu katika nchi hizo ni maskini, idadi kubwa ya watoto ( milioni 18) wenye umri wa kwenda shule hawaendi shule , rushwa, na ukuaji wa uchumi.

Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Umoja wa Mataifa, kwa kushirikiana na Serikali ya Uturuki na unafanyika nchini Uturuki ambapo ndipo chimbuko la mpango kazi huo uliopitishwa mwaka 2011. Tanzania ambayo ni kati ya nchi 38 kutoka Afrika ambazo zimokwenye orodha ya umoja wa Mataifa kama nchi zilizonyuma kimaendeleo ( LDCs) inashiriki kikamilifu mkutano huo.

Afisa Mkuu wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,Bw. Songelael Shilla akizungumza kwenye mkutano huo kwa niaba ya Tanzania, pamoja na mambo mengine ameelezea jitihada mbalimbali zinazotekelezwa na serikali ikiwa ni sehemu ya mikakati yake ya kuhakikisha kwamba inafunzu na kuondoka katika kundi la nchi zilizonyuma kimaendeleo.

Miongoni mwa juhudi na mikakati inayofanywa na serikali ni pamoja na kuhakikisha inapunguza idadi ya wananchi wake wanaoishi katika umaskini uliopindukia, uboreshaji wa huduma muhimu za kijamii, ambazo ni afya sambamba na upunguzaji wa vifo vya watoto wachanga na wanawake wajawazito,, elimu, ujenzi wa makazi bora, usambazaji wa huduma za maji safi na salama na ujenzi wa miundo mbinu ikiwamo ya mawasiliano.

Katika taarifa yake Tanzania pia imeanisha mafanikio kadhaa katika ukuaji wa uchumi wake huku ikisisitiza haja na umuhimu wa mataifa yaliyoendelea kutimiza ahadi zake katika eneo la misaada ya kimaendeleo hatua mbayo itasaidia kuharakisha nchi maskini kupiga hatua na kuondoka hapo zilipo.

Pamoja na kusisitiza ubia na ushirikiano kutoka mataifa yaliyoendelea, Tanzania imesema bado inaamini kwamba wajibu wa kwanza wa kuondoka katika kundi la nchi maskini au zilizonyuma kimaendelo unapashwa kuwa wa nchi zenyewe zilizonyuma kimaendeleo.

Tanzania pia imewasilisha Taarifa yake ( National Mid –Term Review Report) kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa IPoA.
Afisa Mkuu wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Bw. Songelael Shilla, akizungumza katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa unaofanya tathimini ya utekelezaji wa Mpango Kazi kuhusu Nchi ambazo zimo nyuma kimaendeleo ( LDCs) Mkutano huu wa siku tatu unafanyika Antalya nchini Uturuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...