Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi(Kulia) akijibu maswali toka kwa wadau wa bishara(hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau wa biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis Mwinyimvua na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye(Katikati) akichangia hoja katika mkutano wa wadau wa biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis Mwinyimvua na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi.
 Wadau wa biashara kutoka sekta za umma na binafsi wakifatilia mkutano uliofanyika leo uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara nchini.
 Picha zote na Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.

Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
SERIKALI imedhamiria kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kuongeza uwekezaji na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa Kati.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis Mwinyimvua wakati akifungua mkutano wa wadau wa biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara.

Dkt. Hamis Mwinyimvua amesema Serikali imeazimia kuboresha mazingira ya biashara nchini kwa kuandaa sera ambazo zitawasaidia wafanyabishara kuwekeza katika sekta mbalimbali.  

“Tutahakikisha tunaboresha mazingira ya biashara kwani hakuna uwekezaji utakaowezekana kama mazingira ya ufanyaji wa biashara yatakuwa hayaridhishi.” Alisisitiza Dkt Mwinyimvua.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi amesema kuwa kuna haja ya Taasisi zote za umma na binafsi kufanya kazi kwa pamoja ili kuboresha mazingira ya biashara.

Naye Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imeanza kufanya maboresho katika mazingira ya uwekezaji.

Akifafanua kuhusu maboresho hayo Simbeye alisema kwasasa ujasili wa makampuni unafanyika kwa kutumia mfumo wa kieletroniki ambapo muombaji anaweza kusajili kampuni pasipo kufika katika Ofisi za BRELA katika kipindi cha muda mfupi.

Mkutano huu uliondaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ikishirikiana na Baraza la Taifa la Biashara, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania wakishirikiana na taasisi za umma na binafsi umedhamiria kuwezesha wafanyabiashara na wawekezaji kuwa mazingira mazuri ya kufanya biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...