Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KOCHA wa zamani wa timu ya Simba, Abdallah Kibadeni ameutaka uongozi wa Simba kukiangalia zaidi kikosi kilichocheza mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya timu yake kinachonolewa na Mganda, Jackson Mayanja kwani kama wakiamua kukiangalia kwa muda huu kuelekea msimu ujao wanaweza kuwa na mafanikio kutokana na uwezo waliouonesha.

Kibadeni amesema Simba imebadilika sana kwani kwenye mchezo wa mwanzo  amekutana nayo na siyo ile aliyoizoea inayokuwa na mchanganyoko na wachezaji wakubwa, kikosi hicho kimeonesha mchezo mzuri na uliotulia licha ya kushindwa kutumia vema nafasi walizozipata.

"Endapo viongozi wa timu hiyo wanataka kuwa na timu yenye ushindani basi ni vema kikosi hicho wanatakiwa kukiangalia kwani nina imani itakuwa miongoni mwa timu zitakazokuwa na kikosi tishio,"amesema Kibadeni. Katika mchezo dhidi ya timu yake Simba hawakuwa na kitu cha kupetoteza na walikuwa uwezo mkubwa wa kumaliza wakiwa nafasi ya pili.

"simba wamecheza mpira mzuri sana lakini naweza kusema goli letu la kwanza limeweza kuharibu mipango yao kwa kiasi kikubwa", amesema Kibadeni na dakika zote 90 Simba wamecheza mpira mzuri ukilinganisha na walivyokutana nao katika mechi za awali.

Kibadeni amesema matokeo waliyoyapata hayakuwazuia kupambana na hata walipopata goli kupitia kwa nahodha wake Musa Mgosi lakini wakaendeleza mashambulizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...