Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka akimkabidhi mmoja wa wahanga waliounguliwa maduka yao eneo la maili moja kiasi cha shilingi laki tano ikiwa ni kuwapa msaada wa kuanzia mtaji mwingine alipofanya ziara ya siku moja ya kuwapa pole.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akikagua moja ya sehemu ya vibanda vya biashara vilivyopo katika eneo la maili moja baada ya kuteketea kwa moto na kuweza kuunguza maduka matano moto huo ulizuka hivi karibu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA.
WIMBI la kutokea kwa majanga ya moto bado limeonekana bado kuwa ni tatizo sugu kutokana na kuwepo kwa uelewa mdogo kwa wananchi kuhusiana na namna ya kuweza kuzuia majanga ya moto pindi yananapojitokeza pamoja na kutokuwa na vifaa vya kuzimia.
Hayo yamebainishwa na Afisa uhusiano wa Jeshi la zima moto na uokoaji Mkoa wa Pwani Harryson Mkonyi wakati akizungumza katika mkutano maalumu wa kuwafariji na baadhi ya wahanga ambao ni wafanyabiashara waliounguliwa maduka yao na kuteketeza mali zao zote kwa moto katika eneo la maili moja Wilayani Kibaha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...