Na Anitha Jonas – MAELEZO
Viongozi  wa  Timu ya Michezo Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo wameaswa kuwa wabunifu na kuongeza jitihada za kuunda timu bora za michezo zitakazo jipatia ushindi katika mashindano mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mhazini  kutoka Shirikisho la Michezo,Wizara na Wakala wa Serikali (SHIMIWI) Bw.Brown Nyamtiga mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uchaguzi na washindi kutangazwa. 

“Mkiwa kama Wizara yenye jukumu la kusimamia masuala ya Michezo nchini  ni vyema muwe mfano kwa taasisi zote za serikali kwa kuwa na timu imara zenye uwezo wa kupata ushindi pamoja na hili linawezekana pale mtakapoamuwa kuweka jitihada za dhati katika kusimamia hilo”,alisema Bw.Nyamtiga.

Akiendelea kuzungumza katika uchaguzi huo Bw.Nyamtinga alisema anatambua changamoto ya pesa iliyoko serikalini kwa sasa,hivyo viongozi wanapasawa kuwa wabunifu wa kutafuta vyanzo mbalimbali vya fedha ili kuisaidia serikali suala hilo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Timu aliyeibuka mshindi katika uchaguzi huo Bw.Modest Mfilinge kutoka Utawala alisema katika uongozi wake anatarajia kufanya mageuzi chanya katika sekta ya michezo kwa wafanyakazi wa wizara hiyo ikiwa ni pamoja na kuunda mabonaza yatakayo kuwa yakifanyika kila mwisho wiki.

“Awali ya yote nitafanya jitihada za kutambua wanamichezo katika Wizara na kwa hili naamini ndipo nitakapopata wachezaji mahari watakao unda timu bora ya michezo katika Wizara na kikubwa nitakachohitaji ni ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wenzangu”,alisema Bw.Mfilinge.

 Pamoja na hayo Bw.Mfilinge alisema mabonanza anayotarajia kuanzisha ni endelevu na anaimani kubwa na viongozi wenzake waliyochaguliwa kuwa watashirikiana vizuri na kufanya kazi nzuri yenye kuleta matokeo chanya katika timu ya wizara. 

Hata hivyo uchaguzi huo wa Wizara umesaidia kupatikana kwa viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa Timu Bw.Jackson Manyika kutoka Kitengo cha Uhasibu,Katibu Mkuu Msaidizi Bw.Mfaume Said Mfaume kutoka Utawala,Makamu Mwenyekiti Bw.Francis Songoro,Mweka Hazina Bi. Flora Mwenyembegu, Mjumbe Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa SHIMIWI Bw.Carlos Mlinda pamoja na Wajumbe wa Idara .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...