Mgeni rasmi Dr.Guido Nicolai akifungua hotuba maalumu kuhusu Harambee ya kuchangia hospital ya Mwananyamala nchini Tanzania.Kikundi cha Upendo Womens Group kilichopo nchini Ubelgiji jana tarehe 11.06.2016 walifanya Arambee hiyo kuwasaidia kina mama wanaojifungua katika mazingira magumu nchini Tanzania.
Mweka hazina wa kikundi cha Upendo women's Group Begum Chunny akitoa maelewo mafupi jinsi alivyoenda Tanzania kukagua maendeleo yao yanayopatkana katika kuchangia hospital ya Mwananyamala,kulia ni Mwenyekiti wa kikundi hicho Mrs Theresia Greca. 
Kina mama wa Upendo wakiingia ukumbini kwa shangwe huku wakiimba nyimbo ya kuisifia Tanzania
Burudani ya muziki wa Jazz ilitumbuizwa na kikundi cha  JAIL CITY VETERAN,watu waliburudika sana na muziki huo.
Mmoja wa wawakilishi wa Lions Club Wetteren Rozenstreek ya Ubelgiji akikabidhi hundi  kwa wana  Upendo Women's Group 
Mwakilishi wa Inne wheel wetteren akimkabidhi hundi mwenyekiti wa Upendo Women's Group Mrs Theresia Greca katika kuchangia hospitali ya Mwananyamala nchini Tanzania.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2016

    Asanteni sana kwa moyo wenu na muwape shukurani zetu wadau wenzenu waliochangia na waambieni tunawakaribisha sana Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...