Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakisaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo wakipeana mikono baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo, yenye thmani ya zaidi ya dola za Marekani milioni 300, katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda, Afrika Mashariki na Uhusiano wa Kimataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi (kulia) akisoma Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo nchini na Serikali ya Korea kabla ya kusainiwa kwa hati hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 650, Jijini Dar es salaam
Wajumbe toka Serikali ya Tanzania na Korea wakisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa maafisa wa Korea kuhusu Ushirikiano katika Misaada ya Maendeleo ya Kiuchumi kabla ya kusainiwa kwa Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano yenye thamani ya dola za Marekani Milioni 300, kati ya Tanzania na Korea, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Hamis Shaban (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Ushirikiano wa Kimataifa (Uchumi) wa Korea Weon-Kyoung Jo (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tanzania na Korea baada ya kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...