Katika
kusherekea Siku ya Merit ambayo huadhimishwa kila Julai, 24 ya kila
mwaka, vijana mbalimbali nchini wamekutanishwa kwa pamoja ili kuweza
kujadili kuhusu Maendeleo Endelevu (SDGs) pamoja na kuweka mipango jambo
gani lifanyike ili kuhakikisha kila raia anapata elimu kuhusu SDGs.
Akizungumza
na Mo Blog kuhusu siku hiyo, Mwanaharakati wa Maendeleo Endelevu, Rose
Mmbaga alisema kwa Tanzania mwaka huu wamekutanisha vijana kwa pamoja na
kujadili jinsi gani wanaweza kusaidia watu wengine kujiunga katika
utekelezaji wa Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mwanaharakati
wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akitoa neno la ufunguzi katika
kongamano lililokutanisha vijana ikiwa ni katika kusherekea Siku ya
Merit. (Picha zote na Rabi Hume, MO Blog)
Alisema
pamoja na kukutanisha vijana pia wamekutanisha mashirika mbalimbali ya
ndani na nje ya nchi ambayo yataweza kuelezea jinsi gani yanafanya kazi,
jinsi ambavyo yanaweza kuwasaidia vijana na jinsi ambavyo wanaweza
kusaidiana na Umoja wa Mataifa (UN) ili kutekeleza Mipango ya Maendeleo
Endelevu (SDGs).
"Kwa
mwaka huu tumekutanisha mashirika ambayo yameungana nasi katika
kuadhimisha Siku ya Merit lakini pia tuna vijana ambao wameshamaliza
vyuo kwa sasa wanatafuta ajira, vijana waliomaliza kidato cha sita na
wengine wamemaliza kidato cha nne," alisema Rose.
Mwanaharakati
wa Maendeleo Endelevu, Rose Mmbaga akizungumza katika kongamano
lililokutanisha vijana na kupata elimu kuhusu Mipango ya Maendeleo
Endelevu (SDGs).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...