Rock
City Marathon ilizinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam huku wito
ukitolewa kwa wadau wa mchezo wa riadha kote nchini kuhakikisha
wanafanya jitihada za makusudi kuukomboa mchezo huo uliolipa taifa
heshima miaka ya nyuma.
Akizungumza kwenye
uzinduzi wa mbio hizo kwa niaba ya Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Bw
Nape Nnauye, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Michezo wa Wizara hiyo Bw Alex
Nkenyenge alisema kuna haja ya kuwepo kwa jitihada za makusudi miongoni
mwa wadau wa mchezo huo ili kurejesha makali ya taifa katika riadha
yaliyoonyeshwa miaka ya 1970 na 1980.
Kupitia
mkurugenzi huyo Waziri Nape alitoa wito kwa wadau wa mchezo huo
kuhakikisha wanashirikiana na serikali kuhakikisha changamoto
zinazokwamisha mchezo huo zinatatuliwa ili kuwezesha uwepo wa maandalizi
ya kutosha kwa wanamchezo huo.“Ndio maana
nawapongeza waandaaji wa mbio hizi kwa kuwa wanashikiri moja kwa moja
kukamilisha adhma yetu hii muhimu…kama serikali pia tunaahidi kuendelea
kushirikiana nao,’’ alisema.
Akizungumza kwenye
hafla Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus
International, Bi Elizabeth Riziki alisema mbio hizo zinatarajiwa
kufanyika Septemba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza zikihusisha wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo baadhi
ya nchi za Afrika, Ulaya na Marekani. Alisema mbio hizo
zinazofanyika kwa mara ya nane mfululizo tangu zianze mwaka 2009
zinalenga kutambua na kuinua vipaji vya wanariadha nchini na pia kukuza
utalii wa ndani kupitia sekta ya michezo.
“Rock City Marathon zitahusisha makundi matano yaani mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake, mbio za kilomita 5 kwa ngazi ya ‘corporate’, mbio za kilomita 3 kwa ajili ya walemavu, mbio za kilomita 3 tena kwa ajili ya wazee umri zaidi miaka 55 na kuendelea pamoja na mbio za kilomita 2 kwa ajili ya watoto umri kati ya miaka 7 hadi 19,’’ alitaja.
Alitaja baadhi ya makampuni yaliyojitokeza kudhamini mbio hizo ikiwa ni pamoja na Freidkin Conservation Fund, African Wildlife Trust, Mwanza Hotel, Nyanza Bottlers Limited na kampuni ya Real PR Solution.
“ Pia mbio za mwaka huu zimeboreshwa zaidi kwa kuwa zitaambatana na uwepo wa majiko ya wachoma nyama ili kutoa fursa kwa washiriki kufurahia aina hiyo ya kitoweo pamoja na vyakula tofauti vyenye asili ya mkoa huo…ifahamike lengo la mbio hizi kukuza utalii wa ndani ,’’
Tunawaalika wadhamini waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuzifanya mbio za mwaka huu kuwa bora zaidi,” alisema.Akizungumza
kwenye hafla hiyo mdhamini mkuu wa mbio hizo Bw Pratik Patel ambae ni
Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund( FCF) na
African Wildlife Trust (AWT) alisema wameamua kuwa sehemu ya mbio hizo
kwa kuwa zinaendana na mkakati wao kukuza utalii kwa kulinda maliasili.
“Tunafurahia kuwa sehemu yam bio hizi kwa kuwa lengo lake linaenda sambamba na agenda yetu ya kulinda maliasili na zaidi linaenda sambamba na kampeni yetu ya kupinga vita ujangili inayofahamika kama ‘Okoa Wanyama Wetu; Kataa Ujangili’. Alisema.
Kaimu Mkurugenzi wa idara va Michezo Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Bw Alex Nkenyenge (alieshika mkasi) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Rock City Marathon wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es jana. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka kampuni ya Capital Plus International, Bi Elizabeth Riziki (wa kwanza kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund( FCF) na African Wildlife Trust (AWT), ambao ndio wadhamini wakuu wa mbiohizo Bw Pratik Patel (wa pili kulia), Bi Ombeni Savara katibu Mkuu Msaidizi chama cha Riadha Tanzania (wa kwanza kulia) na Joseph Kahama mwenyekiti wa maandalizi ya mbio hizo.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Joseph Kahama akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.
Mwanaridha mkongwe nchini Bw Juma Ikangaa akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa mbio hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa mashirika ya Freidkin Conservation Fund (FCF) na
African Wildlife Trust (AWT), ambae ndio wadhamini wakuu wa mbio
Kaimu Mkurugenzi wa idara va Michezo Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Bw Alex Nkenyenge akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rock City Marathon.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...