Na Anthony John, Globu ya Jamii 
Goethe Institute, kituo cha utamaduni cha Ujerumani,  kwa kushirikiana na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wameandaa onyesho litaloitwa “Maji Maji Flavour” lenye lengo la kukumbusha na kufundisha historia ya vita hivyo kati ya Tanzania na Ujerumani. 
 Onesho hili litafunguliwa katika ukumbi wa maonesho wa TaSUBA mjini Bagamoyo leo, ambapo Januari 24, 2017 litafanyika Dar es salaam International Academy na Januari 26 mpaka 28 litafanyika Makumbusho ya Taifa na Jumba la Utamaduni jijini Dar es salaam. 
“Maji Maji Flava” ilianza maonesho yake nchini Ujerumani katika miji ya Kassel na Berlin mwezi Septemba na Oktoba mwaka jana na jumla ya maonesho 14 yalifanyika nayo yalipokelewa kwa mapokeo chanya kutoka kwa hadhira”, amesema mwandaaji wa onesho hilo Bw. Isack Peter. Amesema wasanii waliotengeneza kazi hii wana mitazamo tofauti ya kimsingi ya kisanii, kiutamaduni, na kisiasa na kijiografia, na mitazamo hii haitofunikwa bali itawekwa wazi kwa msisitizo kwenye kuongoza namna ya utayarishaji kisanii. 
"Mambo ya kigeni yasiyokuwa ya kawaida yatapambanuliwa na fikra kandamizi na mawazo yanayo kinzana vyote vitachunguzwa na kuelezwa kiusanii’’ amesema Peter

Mwandaaji Isack Peter akizungumzia onesho la "Majimaji  Flava" akiwa na Msanii wa kike atakayeshiriki katika onyesho hilo,Sabrina Ceesay 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...