Madaktari nchini wametakiwa kufanya upasuaji bila kufungua tumbo kwa kinamama mara kinamama wanapolazimika kupatiwa huduma hiyo kwa kuwa ni njia salama zaidi na gharama nafuu. 
Ushauri huo umetolewa lLeo na Profesa Rafique Parker kutoka nchini Kenya katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es salaam. 
Profesa Parker ametoa mafunzo ya kufanya upasuaji bila kufungua tumbo kwa madaktari wa kinamama kutoka hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam. 
 “Madaktari mnapaswa kubadilika na kufanya upasuaji bila kufungua tumbo. Kama hamtaki kufanya hivyo dunia itawacha nyuma kwani upasuaji huu ni wa kisasa, rahisi kuliko wa kufungua tumbo na wa gharama nafuu,”amesema Profesa Parker. 
Amesema kabla ya daktari kufanya upasuaji huo anapaswa kuhudhuria kozi mbalimbali zinazohusiana na upasuaji wa bila kufungua tumbo na kwamba ili wafanikiwe wanapaswa kusoma na kuweka nia ya dhati ya kutoa huduma hiyo kwa kinamama. 
 Profesa Parker amewaeleza madaktari hao kwamba mafanikio ya kufikia kwenye upasuaji huo, hayaji siku moja bali wanapaswa kuweka juhudi na kupenda kujifunza mara kwa mara ili kufikia hatua hiyo ambayo ni msaada mkubwa kwa kina mama wenye matatizo ya uzazi pamoja na magonjwa mengine ya tumbo. 
 “Huwezi kujifunza upasuaji bila kufungua tumbo kwa siku moja, daktari anapaswa kuudhuria semina nyingi na kutumia zaidi ya saa nyingi kufikia mafanikio. Kuna madaktari wengi baada ya kumaliza masomo yao hawasomi vitabu, wanaamini kwamba wanajua kila kitu, lakini si kweli. Mnapaswa kubadilika,” amesisitiza Profesa Parker. 
 Mafunzo hayo yamehudhuriwa na madaktari bingwa wa Muhimbili, hospitali ya Temeke, Tumaini, Aga Khan, Dar Group, Chuo Kikuu cha Muhimbili (MUHAS) na hospitali ya Regency pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru.
 Profesa Rafique Parker akiwaeleza madaktari kutoka hospitali ya Temeke, Muhimbili, Aga Khan, Regency, Tumaini, Dar Group na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili umuhimu wa kufanya upasuaji bila kufungua tumbo (laparoscopy) kwa kinamama wanaopaswa kupatiwa huduma hiyo. Semina hiyo imefanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
 Mkurungezi wa Hopsitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru (kulia) akiwa  namadaktari wengine wakimsikiliza Profesa Parker wakati akitoa mada kwa madaktari jinsi ya kufanya upasuaji bila kufungua tumbo kwa kinamama.
 Profesa  Rafique Parker akiwaleza madaktari hatua za kufuata kabla ya kufanya upasuaji bila kufungua tumbo.

 Daktari bingwa wa kinamama, Dk Tarimo (kushoto) wa Muhimbili akiwa na madaktari wengine kutoka katika hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam.
 Madaktari kutoka katika hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam wakifuatilia somo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...