Msanii wa muziki wa asili nchini Mrisho Mpoto, Ijumaa hii amesafiri mpaka Mkoani Shinyanga kwenda kuwajulia hali watoto wake wawili ambao alijitolea kuwalea. Watoto hao ni Pendo pamoja na Simon ambao wanaishi na albinism katika Kituo cha Buhangija Shinyanga ambacho kinalea watoto wenye mahitaji maalumu.
Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo Sizonje, aliambatana na wadau mbalimbali kutembelea kituoni hapo na kutoa kidogo alichonacho. 
"Kile kidogo kikubwa, nilichopewa na Mh Rais Magufuli, sikusita kusafiri na mpaka Shinyanga kugawana na wanangu Pendo na Simon wanaoishi na albinism hapa shinyanga," alisema Mpoto.
Muimbaji huyo hivi karibuni alifanya show nzuri katika uzinduzi wa Mabasi ya Mwendo Kasi hali ambayo ilipelekea mgeni rasmi ya shughuli hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuinuka akiwa pamoja na Mkamu wa Rais wa World Bank Africa, Makhtar Diop na kuanza kumtuza mahela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...