NA Anthon John, Globu ya Jamii.

UONGOZI wa Shirika la Reli Tanzania( TRL) umewatangazia Wasafiri wote wa treni ya mjini iendayo pugu kuwa safari ya tatu awamu ya jioni itaanza tena siku ya Jumatano januari 25, 2017, Safari hiyo itaanza katika kituo kikuu cha Dar es salaam saa 2:15 usiku na kuwasili pugu saa 3:10 usiku.

 Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkuu wa Usafirishaji wa Reli ya Tanzania TRL Rashid Ng'hwani amesema kuanza tena kwa safari hiyo kunatokana na  kukamilika kwa kazi ya kutandika reli mpya katika eneo korofi kati ya stesheni za Llala block, Posta na Karakata.

  Aidha Ng'hwani amesema kuwa Safari za asubuhi zitaendelea kuwa mbili kwa vile kazi ya utandikaji reli bado haujakamilika.

  "Kazi ya ukarabati huanza kati ya saa 3:15 asubuhi hadi saa 8 mchana kila siku za kazi na inatarajiwa kukamilika baada ya wiki 10 tokea ianze kazi hiyo"amesema Ng'hwani.
 
Sanjari na hayo Kaimu Mkuu huyo wa usafirishaji wa reli  ameongeza kuwa ukarabadi huu utaondoa kero ya vumbi kwa abiria kwenye mabehewa kwani njia yote itawekewa kokoto za kutosha (stone ballast) ambazo hazina vumbi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...