Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Kufuatia kusitisha mkataba wake na klabu ya SønderjyskE ya nchini Denmark aliyokuwa anaitumikia, Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeweka wazi kuwa Emanuel Okwi anaweza kusajiliwa na klabu yoyote nchini lakini hataweza kucheza mpaka msimu ujao.

Hilo limekuja baada ya taarifa kusambazwa kuwa Okwi anaweza kuitumikia tena klabu yake ya zamani ya Wekundu wa Msimbazi Simba katika mechi ya Februari 18 kama Kocha mkuu wa timu hiyo Joseph Omog atapendezewa nae. 

Akizungumza na Globu hii, Ofisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa klabu ya Simba ina uwezo wa kumsajili Mganda huyo kwa kipindi hiki lakini hawataweza kumtumia mpaka msima ujao wa ligi na hilo ni kulingana na kanuni za ligi. 

Lucas amesema kuwa kanuni za ligi haziruhusu kumtumia mchezaji ambaye amesajiliwa katikati ya ligi zaidi ya dirisha kubwa la usajili na dirisha dogo na likishafungwa basi klabu itamsajili mchezaji na hawatamtumia mpaka pale litakapofunguliwa tena. Kutokana na hilo, uwezekano wa Simba kumchezesha Okwi kwenye mechi yao dhidi ya watani wao wa jadi Yanga limeshindikana na zaidi wameambiwa wamsajili kama wanamuhitaji ila watamtumia msimu ujao na si vinginevyo. 

Taaarifa za kuachana na klabu yake, Okwi aliweka wazi kuwa atasema wapi atakapoelekea ila haijajulikana kama atarejea tena Msimbazi kwa mara ya tatu au ataamua kwenda timu nyingine. Ikumbukwe kuwa awali Okwi aliitumika Simba kabla ya kununuliwa na timu ya Etoile Du Sahel ya Tunisia na kwenda kuishia kukaa benchi na kuamua kuachana nao na baadae kusajiliwa na Yanga na kucheza kwa kipindi cha miezi sita kabla ya kurejea Simba na hatiumaye kusajiliwa na timu ya SønderjyskE ya nchini Denmark.


Emanuel Okwi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...