Benny Mwaipaja,WFM-Dar es salaam

SERIKALI imesema kuwa inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta hiyo ili kuharakisha maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya viwanda na biashara.

Hayo yamesema na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha -IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea sana sekta binafsi yenye nguvu na yenye utulivu ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwa njia ya uwekezaji na ulipaji kodi.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, amesema kuwa Shirika lake limeridhika na kiwango kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania miongoni mwa nchi za Afrika na kwamba wanatarajia kuona uchumi huo ukiendelea kukua zaidi kwa ushirikiano na sekta binafsi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiwa katika mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati) pamoja na maafisa waandamizi wa Wizara hiyo wakiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa Tanzania na Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF wakiwa katika mazungumzo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam, ambapo Shirika hilo limeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania ili kufikia maendeleo inayoyatarajia kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake kiuchumi na kijamii.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiagana na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, ambapo IMF, imesifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano, katika kusimamia na kukuza uchumi wa Taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...