Leonce Zimbandu
MPIGACHAPA
Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo ameendelea kusisiti za na kuzitaka
taasisi za serikali, binafsi za uchapishaji kuendelea kujisajili katika
ofisi hiyo na kuepuka usumbufu wa kubainika kwenye msako.
Kauli
hiyo imetolewa baada ya kutoridhishwa na kasi ya kampuni za uchapishaji
zilizojitokeza tangu wito huo utolewe Februari 13, mwaka huu, kampuni
24 tayari zimejitokeza.
Chibogoyo
aliyasema hayo alipokuwa akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati
akijibu swali kuhusu kampuni za uchapishaji zilizotii sharia kujisajili
bila shuruti.
Alisema
amesikitishwa na mwitikio mdogo wa usajili wa kampuni na taasisi za
uchapishaji, hivyo akiwa muungwana ameamua kutumia fursa ya
kuwakumbusha watimize wajibu wao kisheria.
“Inawezekana
katika mkutano wangu sikueleweka vizuri lakini usajili unahusu kampuni
binafsi na serikali kwa lengo la kutambua shughuli zao na kuepuka
kujificha,” alisema.
Alisema
baada ya muda uliotolewa kukamilika na ofisi hiyo ikapata taarifa kuwa
ipo taasisi au kampuni inajihusisha na uchapishaji, Ofisi itachukua
hatua ya kuifuatilia.
Hivyo
kabla ya hali hiyo ya ufuataliaji, itakuwa busara kwa wachapishaji hao
kujisajili ndani ya siku tano zilizobaki tangu wito huo ulipotolewa.
Aidha,
alisema ili kuondoa usumbufu kwa kampuni za uchapishaji za mikoani,
zinaweza kujisajili kwa kupitia mtandao wa Ofisi ya Mpigachapa.
Alisema
Wachapishaji halali watakaojiorodhesha watakaribishwa na kupewa fursa
ya kutoa mawazo ya kuiweka nchi mahali salama kupitia nyaraka.
Hatua
hiyo imechukuliwa ili kuendeleza vita dhidi ya wachapishaji wa nyaraka
bandia kwa kuwasaka nyumba kwa nyumba, iwapo watashindwa kujitokeza na
kujisajili kwa hiari.
Mpigachapa Mkuu wa Serikali,Cassian Chibogoyo akionesha waandishi wahabari (hawapo pichani)
katika moja ya mikutano yake rangi sahihi ya bendera yaTaifa,
kulia ni Afisa Habari wa Idara Habari Maelezo, Frank Shija.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...