Nuru Juma na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
MAKAMPUNI
ya JP Decaux pamoja na International Republican Institute (IRI)
yameandaa Tamasha la waendesha pikipiki linalotarajia kufanyika Mei 13
mwaka huu katika viwanja vya Tanganyika Parkers Jijini Dar es Salaam.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
JP Decaux, Shaban Makugaya wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu maandalizi ya tamasha hilo.
“Lengo
la tamasha hili ni kuweka uamsho, msisitizo na kuendelea kutoa elimu ya
usalama barabarani kwa madereva wa pikipiki na abiria kwa dhumuni la
kuzingatia sheria za usalama kwa matumizi ya barabara pamoja na
kudumisha umoja, ushirikiano na mshikamano katika jamii”. Alisema
Makugaya.Aidha,
Makugaya amesema kuwa, tamasha hilo ni la kwanza kufanyika nchini na
Kampuni hiyo imejipanga kulifanya kila mwaka nchi nzima ambapo jina la
maonesho litabadilika kulingana na mji au mkoa ambao tamasha
litafanyika.
Aliongeza
kuwa usafiri wa pikipiki umekua njia rahisi za kumuwezesha msafiri
kufika haraka hivyo mashirika hayo yameamua kuwakutanisha madereva hao
na kuwapa elimu ya usalama barabarani ili waweze kuepuka ajali za
barabarani zinazosababisha vifo vya watanzania wengi.
Akifafanua
zaidi, Mkurugenzi huyo amesema kuwa waendesha bodaboda watakaoshiriki
katika tamasha hilo ni lazima wawe na leseni na watoke katika vikundi
vyao vilivyosajiliwa na kutambulika kisheria.
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya JP Decaux, Elia Moshi
amesema tamasha hilo litahusisha michezo mbalimbali ikiwemo ya soka kati
ya timu ya trafiki na waendesha pikipiki, burudani ya mziki wa kizazi
kipya, taarabu na singeli pia zitakuwepo ili kuboresha tamasha hilo.
“Tamasha
hili litafayika mkoani Dar es Saaam pekee na linatarajia ushiriki wa
watu kati ya 5000 na kuendelea ambapo mshindi wa kwanza atajipatia
pikipiki pamoja na fedha taslimu na kutakua na zawadi zingine kwa ajili
ya washindi wengine pamoja na washiriki,” alisema Moshi.
Bodaboda
Superstar ni onesho linalojumuisha burudani na elimu ambalo limelenga
kuwaleta pamoja waendesha pikipiki na wananchi ambapo Kauli mbiu ya
tamasha hilo ni ‘Sote ni Ndugu’.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...