Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto  akikagua vichochoro  vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kuingia nchini katika kijiji cha  Mugulika  Kata ya Bwerenyange  wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera. Kamishna Jenerali yuko mkoa wa Kagera kujionea shughuli zinazotekelezwa na Idara yake mkoani humo.
 Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa kwanza kutoka kushoto  akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera  Godfrey Mheluka watatu kutoka kulia  katika kijiji cha Muguluka  Kata ya  Bwerenyange  wilaya ya Karagwe  Mkoa wa  Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.
 Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala wa nne kutoka kulia akiwa katika Mkutano wa Hadhara na baadhi ya Wananchi (hawapo pichani) wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe  Mkoa wa  Kagera.Kamishna Jenerali huyo amefanya ziara katika Vipenyo vinavyotumiwa na wahamiaji haramu kutoka nchini nyingine kuingia Tanzania.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Muguluka Kata ya Bwerenyange wilaya ya Karagwe  Mkoa wa  Kagera wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Idara ya Uhamiaji Dk. Anna P. Makakala katika Mkutano wa Hadhara baina ya wanakijiji hao na Ujumbe huo wa Idara ya Uhamiaji kutoka Makao Makuu ambapo katika Mkutano huo Dk. Makakala  alitoa wito  kwa  wanakijiji hao  kutowahifadhi wahamiaji haramu  kwenye makazi yao sambamba na kuwataka kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola pale wanapogundua kuna mgeni asiyeeleweka na wanamtilia mashaka kwenye makazi yao.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...