Na Michael Utouh

AFISA Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis Lissu ameahidi kutatua kero zote zinazowakabili baadhi ya wamiliki wa Shule Binafsiinafsi wa mkoa huo ikiwemo ya tozo kubwa za biashara zinazotozwa shule hizo .

Pia amewaomba wamiliki wa shule hizo kipindi cha likizo wajitolee kuwafundisha masomo ya sayansi wanafunzi wanaotoka shule za serikali kwa kuwa wana walimu wengi wa masomo hayo.

Ameyasema hayo leo alipokuwa akifungua Mkutano Maalumu uliowakutanisha wadau mbalimbali na wamiliki wa shule zilizopo mkoani humo.Amesema wamiliki wa shule hizo pamoja na shule zao wanapaswa watambaue huduma wanazopewa ni stahiki hivyo ni sawa wanazopatiwa shule za Serikali.

“Natamani kuziona shule zote binafsi zikiwa zinazoongoza kutokuwa na changamaoto zozote kwani tunatambua mchango wa uwekezaji hapa nchini,” amesema.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi nchini (TAMONGSCO), Charles Totela ameishukuru Serikali ya mkoa huo kwani imekuwa ikiwapa ushirikiano wa kutosha.

Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali ya mkoa huo kuwaundia dawati la pamoja litakalowakutanisha viongozi wote wa shule binafsi, za serikali na watendaji wao ili waweze kukaa pamoja na kujadiliana baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa hazifanyiwi kazi.

Naye Mkurugenzi wa Shule za Al-Muntazir, Mahmood Ladack amewashukuru wamiliki wa shule hizo kwa kuhitisha mkuatano huo ambao anataraji utakuwa na manufaa makubwa kwao na taasisi wanazosimamia katika kupambana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Afisa elimu wa mkoa wa Dar es salaam akizungumza na washiriki wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa shule binafsi mkoa wa Dar es Salaam
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa shule binafsi (TAMONGSCO), Charles Totela Akizungumza 
Miongoni mwa wamiliki wa shule binafsi pamoja na wawakilishi waliofika kwenye mkutano huo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...