Zaidi ya wanahisa 1500 wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC,Walikutana kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki na kufanya mkutano  na Uongozi wa kampuni hiyo na  kuchagua viongozi mbalimbali na kufikia mwaafaka wa gawio la kwanza la Hisa kwa wanachama hao utakaotolewa na kampuni hiyo  kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 26 ifikapo mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu. 
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam,na Mwenyekiti wa Bodi ya Vodacom Tanzania PLC, Ali Mufuruki alipokuwa akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na utoaji wa gawio hilo kwa wanahisa wake. 
Mwenyekiti huyo wa bodi alisema kwamba kila mwana hisa atapatiwa gawio hilo la shilingi 12 na senti 74. 
Aidha alisema kampuni hiyo imeamua kufanya hivyo kutokana na kuimarika vizuri kwa kujiendesha kibiashara hivyo iliona ni vyema kutoa gawio hilo, ili kila mwanahisa aweze kunufaika pale inapobidi. 
Kampuni hiyo pia iliweza kufanya mkutano wake Mkuu wa mwaka kwa kuwakutanisha wanachama wake kutoka mikoa mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo pamoja na kwenda sambamba na uteuzi wa wajumbe wapya watakaoingia ndani ya bodi ya wakurugenzi. 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Ian Ferrao  aliwapongeza wajumbe wote walioteuliwa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa lengo la kuhakikisha hisa za vodacom zinaleta manufaa kwa wamiliki wake wote. 
“Wanahisa watoe shaka kabisa kuhusiana na hisa zao kwani zipo salama na kampuni inaendelea kufanya vizuri sokoni na ninawapongeza wajumbe walioteuliwa na ninaimani nayo  kwani itafanya kazi kwa kushirikiana vizuri  na wanachama ndani nasi tutawapa ushirikiano wakutosha ndani ya kampuni yetu”, alisema Ferrao. 
Mkutano huo mkuu wa mwaka umefanyika kwa mara ya kwanza kwa wanachama wake tangu kampuni hiyo iuze hisa zake kwa Umma. 
 Baadhi ya wanahisa wa Vodacom Tanzania PLC wakifuatilia mada wakati wa mkutano mkuu  wa kwanza  wa wanahisa hao uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wanahisa wa Vodacom Tanzania PLC wakifuatilia mada wakati wa mkutano mkuu  wa kwanza  wa wanahisa hao uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mmoja wa wanahisa za Vodacom Tanzania PLC ,akichangia mada wakati wa mkutano mkuu  wa kwanza wa wanahisa hao  uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Baadhi ya wanahisa za Vodacom Tanzania PLC,wakibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa  Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kulia)wakati wa mkutano mkuu  wa kwanza wa wanahisa hao  uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Tanzania PLC, Ali Mufuruki (kulia) akisalimiana na mmoja wa wanahisa wa kampuni hiyo, Adella Kaale,wakati wa Mkutano  mkuu wa kwanza wa wanahisa hao uliofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari( hawapo pichani)  juu ya Mkutano mkuu wa kwanza wa wanahisa wa kampuni hiyo  uliofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Katikati ni Mwenyekiti wa bodi wa kampuni hiyo, Ali Mafuruki na Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni hiyo, Jacgues Marais

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...