Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

RAIA wawili wa Somalia na Mtanzania mmoja, leo Novemba 23, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi na kuisababisha serikali  hasara ya Sh milioni 370.1.

Wakili wa serikali Jehovaness Zacharia amewataja washitakiwa hao kuwa ni, Mahad Ahmad Salat (30) mfanyabiashara na Mkazi wa Temeke,  Faudhia Abdi (31) mfanyakazi wa ndani na Ally Yusuf (22) Mwanafunzi na Mkazi wa Temeke.

Washtakiwa hao wamesomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.Wakili Jehovanes amedai Agosti, mwaka huu  jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Salat aliingiza vifaa vya kielektroniki nchini pasipo kuwa na leseni kinyume na sheria.


Alidai washitakiwa hao waliingiza vifaa viwili vya mawasiliano ya Kimataifa vyenye namba za utambulisho DB 17-5060-1400=0269 na DB 27-6220-1860-0023 bila kuwa na leseni  kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Pia alidai kabla ya Agosti 25, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa Salat aliunganisha vifaa viwili mawasiliano vya kielektroniki bila kuwa na leseni  ya TCRA.

Aidha katika shtaka la tatu, alidai washitakiwa wote kwa pamoja kati ya Agosti 25, na Oktoba 31, mwaka huu, Dar es Salaam, waliendesha mitambo ya mawasiliano ya Kimataifa kwa ajili ya kupokea mawasiliano bila kuwa na leseni.

Zacharia alidai kati ya Agosti 25 na Oktoba 31, mwaka huu jijini  Dar es Salaam, washtakiwa walikwepa kufanya malipo ambayo yalipaswa kufanyika kwa kuruhusu mawasiliano nje ya nchi kutokana na kutumia kifaa hicho cha mawasiliano bila kuwa na leseni.Aidha, Washtakiwa kinyume na sheria walitumia vifaa vya mawasiliano vilivyounganishwa na vifaa vingine vya mawasiliano kwa nia ya kupokea mawasiliano bila kupata uthibitisho kutoka TCRA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...