Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

Kampuni ya Simu ya TTCL nchini, leo imazindua mpango mkakati wa mageuzi ya kibiashara unaolenga kuirejesha kampuni hiyo kuwa kiongozi wa huduma za mawasiliano (Tehama) katika soko la ndani ya Tanzania na nje.

Mpango huo ambao umezinduliwa jijini Dar es Salaam na Afisa Masoko Mkuu, wa kampuni hiyo, Laibu Leornad ambapo pamoja na mambo mengine, uzinduzihuo unajumuisha matumizi ya teknolojia ya kisasa ya 2G, 3G na 4G, huduma itakayopatikana katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani na Dodoma.

Aidha ametaja mikoa mingine ni Kigoma, Mtwara, Tanga, Zanzibar, Shinyanga, Mwanza, Arusha, Mbeya, na Iringa na Tabora.Akizungumza na waandishi wa habari Leonard, alisema lengo ni kuona wanatoa huduma bora kwa wananchi.“Na hivi sasa tunaendelea kutoa huduma mbalimbali za mawasiliano kwa njia ya sauti pamoja na data kwa gharama nafuu na tumeshuhudia wananchi wengi wameanza kurudi nyumbani kutokana na ubora wa vifurushi, gharama nafuu, na huduma nyingine,” alisema Leonard.

Alivitaja vifurushi ambavyo TTCL imevizinduwa kuwa ni pamoja na Kifurushi cha Bandika Bandua;ambacho kinatoa fursa kwa wateja kutumia intaneti kwa kiwango fulani kuanzia 12:00 asubuhi – 04:00 usiku na kiasi kikubwa wakati wa Usiku kuanzia 04:00 usiku -12:00 asubuhi.

Kingine ni kifurushi cha T.Connect plus; ambacho kimeboreshwa zaidi kwa kutoa fursa kwa wateja kuendelea kufurahia huduma ya mawasiliano kwa gharama nafuu na GB za kutosha. Alisema mteja atakayenunua kifurushi cha Siku, Wiki na Mwezi atapata zaidi ofa ya kutumia Intaneti bure kuanzia majira ya 12:00 asubuhi -03:00 asubuhi.

“…Kifurushi cha Waandishi;- TTCL  ni cha kwanza katika historia ya nchi yetu, “TTCL tunatambua umuhimu mkubwa wa waandishi wa habari katika nchi yetu, sekta hii ya Habari imekuwa na mchango mkubwa kuleta maendeleo kwa wananchi.”amesema.

Ofisa Mkuu Mauzo na Masoko wa Kampuni ya TTCL, Laibu Leonard akizungumza leo Dar es Salaam na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya za mawasiliano ya Intaneti (Data) kwa wateja zenye ofa kabambe za muda wa kutosha kupiga simu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...