Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Dk. Juma Ali Malewa amepokea utambulisho
wa Mwalimu wa Judo Shozy Yogi aliyekuja kumtembelea Makao Makuu ya Magereza
jijini Dar es Salaam leo tarehe 06 December 2017.
Mwalimu Shozy Yogi alifika Makao Makuu ya Magereza akiambatana na kiongozi wa
Japan International Cooperation Mr. Tsujimoto Makoto, Mkuu Msaidizi wa Kikosi
Maalum cha kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM), Mrakibu Alli Uwesu na Msaidizi wa
Mwalimu, Warder Oscarius.
Kamishna Jenerali Malewa aliupokea ugeni huo na kufanyanao mazungumzo ya jinsi
mwalimu huyo ataendesha mafunzo hayo kwenye kambi ya KMKGM.
Mwalimu Shozy Yogi aliwasili toka tarehe 17 November,2017 na amefika hapa
Tanzania kwa mafunzo ya muda mrefu ya mchezo wa Judo kwenye kambi ya Kikosi
Maalu cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKGM)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Dk. Juma Malewa akimsikiliza Kiongozi
wa Japan Internation Cooperation (JICA) Mr. Tsujimoto Makoto alipomtembelea ofisini
kwake.
Mwalimu wa mchezo wa Judo toka Japan, Shozy Yogi(Kushoto) akimsikiliza
Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa (hayupo pichani) alipotembelea Makao Makuu ya
Magereza. Kulia kwake ni kiongozi JICA ambaye amemleta Tanzania.
Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa(wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Mwalimu Shozy Yogi(mwenye shati jeupe), Mr. Tsujimoto Makoto (mwenye
suti nyeusi), Kamishna wa Utawala na Fedha(wa tatu kushoto). Wengine ni Mrakibu
Mwandamizi Matilda Mlawa (wa kwanza kushoto), Mrakibu Alli Uwesu na Wdr
Oscarius.
Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa akiagana na Mwalimu wa Judo Shozy Yogi
ofisini kwake baada ya kufanya nae mazungumzo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...