Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi waliochaguliwa kuongoza kwa kuzingatia Katiba, Kanuni za UWT, CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

Makamu wa Rais aliwasihi viongozi hao kuvunja makundi ya kampeni nwaliyokuwa nayo na kujenga Umoja na Mshikamano ndani ya Jumuiya na Chama.Makamu wa Rais alisisitiza kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na kwa uzalendo “Kushinda kuwa Kiongozi haina maana unajua yote, tuwe tayari kukosoana lakini tusisingiziane”

Makamu wa Rais aliwakumbusha Viongozi hao kuhakikisha Jumuiya inashiriki kikamilifu katika kuandaa mazingira mazuri ya ushindi wa CCM katika chaguzi za Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu 2020.Makamu wa Rais alisema Viongozi waliochaguliwa wanajukumu kubwa la kujenga Jumuiya imara kwa kuitoa hapo ilipo na kuipeleka mbele ikiwa na kuongeza wanachama wapya kutoka katika makundi mbali mbali.

Mkutano Mkuu wa Tisa wa UWT ulifunguliwa jana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kufungwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambapo ulifanyika uchaguzi na Mhe. Gaudensia Kabaka alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Wanawake Tanzania na Bi. Thuwayba Kisasi alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akihutubia wakati wa kufunga mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka baada ya kutangazwa mshindi katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT, uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo aliwasihi uchaguzi umeisha waimarishe Jumuiya hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akimpongeza Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo aliwasihi uchaguzi umeisha waimarishe Jumuiya hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akiwapungia mkono wajumbe wakati wa kufunga mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania Ndugu Gaudensia Kabaka akihutuba baada ya kuchaguliwa katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya wadhamini wa UWT akiwa kwenye picha ya pamoja na wagombea waliogombea nafasi ya Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania katika mkutano mkuu wa tisa wa UWT uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete mjini Dodoma ambapo aliwasihi uchaguzi umeisha waimarishe Jumuiya hiyo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...