Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira Anthony Mavunde amewataka vijana wasomi wa nchi kuwa mstari wa mbele kuunga mkono kazi nzuri na kubwa anayofanya Rais John Magufuli katika kupambana na Rushwa, Ufisadi na Udhalimu.

Mavunde ameyasema hayo jana katika ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre-Dar es salaam wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya Viongozi wa Vyuo vikuu nchini juu ya masuala ya Maadili ya viongozi na rushwa.

Amehimiza Vijana wasomi kutambua nafasi yao katika Jamii na kutambua kwamba Taifa hili linawategemea kwa ustawi wake hivyo lazima wawe mstari wa mbele kuhakikisha kwamba tunajenga Taifa la Vijana wenye maadili lakini pia Vijana ambao watakuwa mstari wa mbele katika kupambana na Rushwa na aina yoyote ya udhalimu.

Aidha,Mwenyekiti wa Tahliso Stanslaus Peter Kaduguze amewashukuru Taasisi ya Uongozi kwa kufanikisha mafunzo hayo ambayo anaamini yamebadilisha fikra na mtizamo wa Vijana wengi wasomi juu ya masuala ya Maadili na Vita dhidi ya rushwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...