Na Wankyo Gati, ARUSHA

Mkazi wa Mtaa wa Jamhuri kata ya Daraja Mbili Halmashauri ya Arusha Mjini Mkoani hapa, Asha Hussein amewaomba Wananchi kumsadia Fedha za Matibabu na kujikimu kimaisha kutokana na tatizo la Ugonjwa wa Utindio wa Ubongo aliyepata Mtoto wake Abul Hussein (6).

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwao , Mama Mzazi wa Mtoto huyo, alisema kuwa Mtoto wake kwa kipindi cha Miaka Minne tangu kuzali kwake amekuwa akitumia Mirija ya mipira wakati wa kula chakula kutokana na hali ya Ugonjwa inayomkabili kwa sasa.
Aliongeza kuwa anawaomba Watanzania kunisaidia ili niweze kupata Matibatu ya Mtoto sababu hali yake ni Mbaya sana nayakuuzunisha, suala la uchumi ni ngumu hata kupata Fedha za kumshughulikia katika Matibabu limekuwa ni shida kwa kweli”

Akizungumzia hali ya Ugonjwa kwa Masikitiko, Mama wa Mtoto huyo, alisema kuwa kwa kipindi cha miaka Minne Mtoto wake amekuwa akiishi ya kulishwa chakula kwa kutumia mirija, hali inayosababisha kutapika kila Mara na wakati mwingine damu umtoka kutokana na mipira hiyo kukaa tumboni kwa muda mrefu. Alisema kuwa Mtoto huyo alipozaliwa alibainika kuwa alikuwa na tatizo la kukakamaa na kutokuona vizuri ambapo alisema kitaalamu tatizo hilo, linaitwa tatizo la utindio wa ubongo.

Kwaupande wake daktari bingwa Julius Msuya wa magonjwa ya kina mama na watoto kutoka hospitali ya St Thomas Mkoani Arusha alisema kuwa hali hiyo inatokana na uchelewaji wa mama kujifungua ambapo husababisha kukosekana kwa hewa ya oksijeni katika ubongo wa mtoto na hivyo kupelekea kupata matatizo mbalimbali ikiwemo kutokukomaa kwa viungo vyake sanjari na kupata tatizo la utindio wa ubongo.

Msuya alisema kuwa wakati wakujifungu kwa kinamama ikitokea kama kachelewa ndiyo matatizo kama hayo, yanamtokea Mtoto na kumsababishia Madhara Makubwa . Amina Salum ni Jirani, na yeye alitoa angalizo kwa wanawake na watoa huduma wote wa hospitali hapa, Nchini kuwa makini ili kuepusha upatikanaji wa watoto wa aina kama ya Abdul.

Alieleza kuwa Kumekuwepo na ongezeko la watoto wa aina hiyo katika jamii hali ambayo imekuwa ikizua taharuki katika familia na wengine kuhusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina badala yake wakina mama wajawazito wametakiwa kuchukua tahadhari juu ya suala hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...