Na Judith Mhina - MAELEZO

Mojawapo ya sababu zinazowakosesha Wakulima kupata mazao mengi shambani ni viumbe hai waharibifu ambao hushambulia mbegu au mazao yenyewe kabla na baada ya kuvunwa. 

Kutokana na hali hii uzalishaji wa mazao shambani unapungua na pia kiasi kidogo kinachopatikana baada ya kuvuna nacho hupungua kutokana na viumbe hao waharibifu kuendelea kuharibu kikiwa ghalani. Aidha, hali hii kuwakosesha Wakulima kipato chao na Taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa mtafiti kutoka Kituo cha Viumbe Hai Waharibifu wa Mazao na Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, Dkt. Christopher Sabuni, aliyenukuliwa kupitia kipindi cha "Ukulima Bora" kinachorushwa na TBC FM, viumbe hai waaribifu wa mazao wapo wengi na wamegawanyika katika makundi tofauti kama vile wanyama, wadudu, na ndege.

Amewataja viumbe hai waharibifu katika mazao ya kilimo wanaotambulika sana na wakulima hapa nchini ni pamoja na panya, kupe, dumuzi, mdudu Cytophilus au tembo, viroboto, kupe, mmbu na wengineo.Amesema, jukumu la Kituo cha Viumbe Hai Waharibifu wa Mazao ni pamoja na kufanya tafiti mbalimbali zitakazosaidia kuokoa mazao ya wakulima yasiharibiwe na wadudu ili kumwezesha mkulima kupata mazao mengi zaidi.

Kutokana na jukumu hilo, Kituo hicho kimefanya utafili wa kudhibiti panya waharibifu wa mazao ambapo kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo asilimia 40 ya mazao mashambani yataokolewa. Dkt. Sabuni amesema utafiti huu una manufaa mengi kwa mkulima ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya ufundishaji na udhibiti wa uharibifu wa mazao. 

"Hata hivyo, tunalenga kutoa elimu kwa mkulima ni kwa jinsi gani anaweza kupunguza hasara ili aweze kufaidika na nguvu zake kwa kuvuna chakula kingi iwezekanavyo,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...