Na Ripota , Globu ya jamii .

CHAMA cha Wananchi(CUF) kimesema kimejipanga vema kuhakikisha wanashinda uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku kikionesha kutokuwa na wasiswasi na mgombea wa Chadema Salum Mwalimu ambaye amejitosa kwenye uchaguzi huo. 

Kauli ya CUF inakuja siku moja tu baada ya Mwalimu ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema upande wa Zanzibar kuchukua fomu ya kugombea ubunge Kinondoni. 

Akizungumza na Michuzi Blogu leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF , Abdallah Kambaya amesema wao walishajipanga na kuweka mikakati ya kushinda uchaguzi huo kupitia Salim Jumaa . 

Amefafanua tangu mwanzo walishasema wataingia kwenye uchaguzi huo kwani wanajua jimbo la Kinondoni ni ngome ya CUF na hivyo hakuna wa kuwasumbua. 

"Tumejipanga mapema na tumeona Salum Mwalimu amechukua fomu ya kugombea ubunge na tayari kairudisha huku akisindikizwa na safu ya viongozi wake. Tulitarajia Mwalimu atachukua fomu na ndicho alichofanya. 

"Kwetu sisi wala hakuna ambacho tuna hofu.Hawatumiizi kichwa,"amesema Kambaya na kuongeza CUF imekamilisha kila idara kuhakikisha wanashinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...