Halmashauri ya Mji wa Babati inaendelea na zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea; ambapo wananchi wamehamasika na kujitokeza kwa wingi kusajiliwa.

Akizungumzia zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati Ndg. Fortunatus Fwema amesema kiujumla zoezi la Usajili katika Halmashauri yake linaendelea vema isipokuwa changamoto za hapa na pale.

Amezitaja baadhi ya changamoto ni ushiriki hafifu wa wananchi kutokana na msimu wa kilimo asilimia kubwa ya wananchi kuwepo mashambani, mvua na uelewa mdogo wa wananchi katika masuala yanayohusu umuhimu wa Vitambulisho.

Amewataka Wananchi kugawa muda wa kilimo na wa kujiandikisha ili waweze kutumia fursa hii kujisajili na kuagiza watendaji wote walio chini yake kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hili.
Wananchi wa Kata ya Babati mkoani Manyara wakiwa wamepanga foleni ya kuingia katika chumba cha Usajili wa Vitambulisho vya Taifa.
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Babati Ndg. Fortunatus Fwema akielezea umuhimu wa Kitambulisho cha Taifa kwa wananchi ikiwa ni kutambulika na kupata huduma za kijamii kirahisi pamoja na kuwezesha Halmashauri yake kuwa na takwimu sahihi zitakazowasaidia kupanga maendeleo kwa wanannchi wao kwa urahisi alipohojiwa na waandishi wa Radio Manyara. 
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Babati Ndg. Fortunatus Fwema akifanya mazungumzo juu ya maendeleo ya zoezi wakati Afisa Msajili Mkoa wa Manyara kutoka NIDA alipofika ofisini kwake kwa mazungumzo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...