*IGP Sirro asema wahalifu Kibiti wakimbilia Msumbiji

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
JESHI la Polisi nchini Tanzania na Jeshi la Polisi Msumbiji wamesaini makubaliano ya kushirikiana kukabiliana na uhalifu katika nchi hizo huku akieleza kwa sasa Kibiti ni salama.
Utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano huo umefanywa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro na Msumbiji umefanywa na Mkuu wa Jeshi la Polisi la nchi hiyo Bernardino Rafael.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, IGP Sirro amesema katika kupambana na uhalifu kwenye nchi hizo pia watakuwa wanabadilishana taarifa na kudhibiti utakatishaji fedha.

Amefafanua mbali ya kudhibiti matukio ya utakatishaji fedha,pia watakomesha biashara haramu ya dawa za kulevya, matukio mengine ya uhalifu.
Ameongeza kuna taarifa baada ya Polisi nchini kudhibiti wahalifu waliokuwa Kibiti, Ikwiriri kuelekea hadi Mtwara baadhi yao wamekimbilia Msumbiji.
Amesema taarifa zilizopo zinaonesha tayari kuna watu wanne wamefariki dunia nchini Msumbiji na walikuwa wanazungumza Kiswahili.

"Wengi ambao wametoroka huku kwetu baada ya kuwadhibiti waliamua kukimbilia nchi ya Msumbiji.
"Tumedhamiria kupambana na kila aina ya uhalifu kwa nchi zetu.Lengo letu Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla iwe salama na tulivu,"amesema IGP Sirro.
Ameongeza mwenzako anapokuwa na shida ukiiacha hiyo shida itakurudia hivyo wamekubaliana kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Pia amesema wale wahalifu wa kutoka Kibiti na Ikwiriri waliokimbilia Msumbiji, Kongo, Rwanda na nchi nyingine, baadhi ya nchi hizo wamesha saini mkataba wa makubaliano ,hivyo watapatikana.

 "Hivyo wajue hata huko walikokwenda hawako salama kwani watashughulikiwa.Ni vema wakaacha uhalifu,"amesema.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Msumbiji, Rafael amesema makubaliano hayo yatasaidia kudhibiti uhalifu yakiwemo makosa yanayovuka mipaka na kuzifanya nchi hizo kuwa salama.
"Tunataka nchi zetu ziwe salama na kwa makubaliano ambayo tumeingia leo hii yatasaidia kukomesha matukio ya uhalifu na wahalifu,"amsema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...