Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kiliunganishwa na Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar cha Chwaka, Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar cha Maruhubi na Chuo cha Afya cha Mbweni kwa sheria No. 7 ya mwaka 2016
Kutokana na muungano huo, majina ya taasisi hizo yamebadilika na kua kama inavyoonekana kwenye jadweli hapa chaini

  S/NO
JINA LA ZAMANI
JINA JIPYA
     1
Chuo cha Uongozi wa Fedha Zanzibar
Skuli ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.
     2
Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar
Taasisi ya Utalii ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
     3
Chuo cha Afya
Skuli ya Afya na Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar

Hivyo, mawasiliano yote yanayohusu taasisi hizi yapelekwe kwa anuani ifuatayo:-

Makamu Mkuu wa Chuo
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
S.L.P. 146
Tunguu – Zanzibar.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...