Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ali Hapi amepongeza utendaji wa Mamlaka ya Maji
Safi na Maji Taka Dar es Salaam DAWASA na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa
miradi ya Maji Taka katika Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali
kuhakikisha kuwa Wananchi wanapata huduma Bora.
Akizungumza wakati wa ziara yakukagua maeneo yenye changamoto za majitaka na
mradi wa uboreshaji wa huduma za maji taka ili kujionea hatua iliyofikiwa na DAWASA
katika kutekeleza miradi hiyo Mhe. Hapi amesema kuwa ameridhishwa na kazi
inayofanywa na Mamlaka hiyo katika Wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya Habari iliyotolewa na Mamlaka hiyo bomba
lenye jumla ya kilomita 563 litajengwa ili kusafirishia maji taka hadi kwenye mitambo
mikubwa itakayojengwa Mbezi beach, Jangwani na Kurasini jijini Dar es salaam.
Mtambo utakaojengwa eneo la Kilongawima utakuwa na uwezo wa kusafisha lita za
ujazo 16,000 kwa siku na utajumuisha mfumo wenye urefu wa kilomita 97
utakojengwa katika eneo la mbezi Beach, Kawe, Tegeta na maeneo ya jirani na
kutekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia na
unatarajiwa kugharimu dola za Marekani milioni 65.
Mradi mwingine ni ule wa ujenzi wa mtambo wa kusafisha mita za ujazo 11,000 kwa
siku utakaojengwa Kurasini ukihusisha maeneo ya Keko, Changombe, Kurasini, Temeke
na Uwanja wa Taifa ambapo mfumo wake utakuwa na urefu wa kilomita 90.
Aidha, katika eneo la Jangwani mtambo wenye uwezo wa kusafisha lita za ujazo
200,000 kwa siku utajengwa ambapo mabomba yatalazwa kutoka Ubungo,Kinondoni,
Mwanenyemala, Msasani, katikati ya Jiji na Ilala hadi Jangwani ambapo awamu ya
kwanza ikikamilika itahusisha mtambo wa kusafisha kiasi cha lita za ujazo 25,000 za
maji taka kwa siku.
Mradi huo katika eneo la Jangwani utagharimu dola za marekani milioni 90 ambapo
taratibu za manunuzi zinaendelea ili kumpata mshauri na hatimaye mkandarasi, lengo
ni kuanza kwa ujenzi huo mapema mwaka huu.
DAWASA imekuwa ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wakuu wa
Wilaya katika kutekeleza majukumu yake ya kutoa huduma bora kwa wananchi kwa
kuzingatia dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa Mamalaka ya Majisafi na
Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) Modester Mushi akitoa maelezo kwa
Mkuu wa Wilaya Kinondoni Ali Hapi kuhusu mradi wa ujenzi wa mtambo wa
kusafisha Majitaka, Jangwani Beach, Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO), Shabani Mkwanya, wakati akikagua mashine ya kusukuma majitaka, na mradi wa ujenzi wa mtambo wa kusafisha majitaka unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka DaresSalaam (DAWASA).
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akizungumza mara baada ya kukagua mashine ya kusukuma Majitaka katika eneo la Msasani Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) Shabani Mkwanya wakati akikagua chemba za Majitaka katika eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Fundi wa DAWASCO akifunua chemba wakati Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi (mwenye suti nyeusi) akikagua chemba hiyo katika eneo la Msasani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...