Power on Fitness Gym iliyopo Mwenge, kinondoni, Jijini Dar es salaam imeukaribisha mwaka 2018 kwa style ya kipekee ambapo wadau mbalimbali wamejumuika kufanya mazoezi pamoja na kuburudika kwa chakula, Vinywaji na muziki kabambe wa Skylight Band.

Shughuli hiyo imefanyika Jumamosi January 27,2018 katika viwanja vya posta vilivyopo Sayansi, Kijitonyama. Shughuli hiyo ilianza saa 12 asb na inatarajia kumalizika usiku mnene.

Siku hiyo imepambwa na mazoezi ya kukimbia(Jogging) ambayo yameanza alfajiri ya saa 12, na kufuatiwa na mazoezi ya Aerobics, Steps, Zumba, Mpira wa miguu, na michezo mingine kama kuvuta Kamba, Kukimbiza Kuku nk.

Baada ya mazoezi kukamilika wadau wa Power on Fitness Gym wamejumuika katika burudani kabambe ya muziki iliyoporomoshwa na bendi ya Skylight na Ma DJ wakali wa hapa nchini.

Siku hiyo pia kutakuwa na Nyama choma itakayoandaliwa kiufundi na wapishi waliobobea, Supu bila kusahau vinywaji vya kila aina.

Shughuli hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya JSP Marketing Link Limited ikishirikiana na Msouth Company, Dagaa Microfinance Limited, Simba Makini Group, Jaina Ice Cubes, Micgen Insurance Brokers, TTCL na wenyeji Power on Fitness Gym.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...