Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kalambo pamoja na kamati yake ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kalambo kukaa pamoja na kuandaa mkakati wa kuzui uvuvi haramu unaoendelea katika mwambao wa ziwa Tanganyika ili kuokoa viwanda vilivyopo katika mwambao huo.

Amesema kuwa uvuvi haramu unaoendelea katika mwambao huo unahatarisha maendeleo ya viwanda vya samaki vilivyopo na hatimae kudhoofisha ajira za wananchi waliopo karibu na viwanda hivyo na hatimae kurudisha nyuma juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuibua na kuimarisha viwanda vilivyopo.

“Mwisho wa mwezi huu nataka taarifa ya namna mlivyojipanga kupiga marufuku uvuvi haramu ikiwa ni pamoja na kutoa elimu na kuwakamata wale wanaokaidi na kuendesha uvuvi haramu, uvuvi haramu ukiendelea hiki kiwanda hakitakuwepo, kwasababu ya kuua samaki na watoto wake, achene uvuvi haramu, mnamaliza samaki katika ziwaletu hili,” RC Wangabo Alisisitiza

Ameongeza kuwa samaki ndio rasilimali pekee inayowaajiri pamoja na kuendesha kiwanda na kuwataka wananchi kuungana pamoja kuhakikisha wanatunza rasilimali hiyo, na kupiga marufuku aina zote za uvuvi haramu na kuonya kutosikia kiwanda kimefungwa kutokana na kukosa samaki amabao wamekwisha kwasababu ya uvuvi haramu.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kutoka kulia) akipewa maelezo na Mkurugenzi wa Mikebuka Fisheries Tanzania Ltd Azim Premji (wa pili kutoka kulia) katika kiwanda cha Mikebuka Fesheries Tanzania Ltd.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo akipiga marufuku uvuvi haramu katika ziwa Tanganyika ili kuokoa viwanda vilivyopo katika mwambao wa Ziwa hilo, (kushoto aliyekaa) Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh. Julieth Binyura.  
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mhandisi Mshauri, Martin Hossey (wa pili kushoto) kuotoka Kampuni ya Nicholas O'Dwyer inayosimamia ujenzi wa Barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga yenye urefu wa Km 112 ya thamani ya Bilioni 133 iliyomalizika kwa kiwango cha Km 71.5. 

Mwonekano wa Kiwanda cha Akwa Fisheries Tanzania Ltd kilichosimamisha uzalishaji. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...