NA WAMJW-DAR ES SALAAM


SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imeandaa Muongozo wa matibabu nchini na orodha ya dawa zote muhimu ili kuepukana na tatizo la usugu wa vimelea vya dawa. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote muhimu uliofanyika leo jijini Dar es salaam. 

Ni muhimu kila kituo cha afya kuwa na dawa za kutosha, vifaa na vifaa tiba lakini ni lazima tuzingatie muongozo wa matibabu na orodha ya dawa kulingana na ugonjwa fulani ili kuepuka tatizo hili" alisema Waziri Ummy,

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Muongozo huo umezingatia vigezo vyote vya kuweka dawa ambazo zilikuwa hazipo katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya ambazo zimepata uthibitisho kutoka Shirika la Afya la Dunia (WHO). 

Aidha Waziri Ummy amewapiga marufuku Bohari Kuu ya dawa ya Taifa MSD na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) kuagiza na kuandika dawa zilizo nje ya muongozo uliozinduliwa leo ili kuondoa matumizi ya dawa yasiyo sahihi. Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa kila kituo cha afya ni lazima kiongozwe na Tabibu na sio vinginevyo ili kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana katika kituo cha afya husika. 

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa itafika kipindi vituo vya afya ambavyo havikizi vigezo vitafungiwa ili kuepuka usababishwaji wa vifo visivyo vya lazima kwa watanzania. Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi amesema kuwa muongozo wa kutibu magonjwa mbambali umezingatia Orodha ya dawa ambazo zitakuwa zinatumika nchini kwetu kama dawa muhimu za kutibu magonjwa hayo. 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Muongozo wa Matibabu na Orodha ya dawa muhimu wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali prof. Mohammed Bakari Kambi na kushoto ni Mwakilishi wa WHO.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Muongozo wa Matibabu na Orodha ya dawa muhimu wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali prof. Mohammed Bakari Kambi na kushoto ni Mwakilishi wa WHO.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa Muongozo wa matibabu na orodha ya dawa zote muhimu leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto mwenye kilemba akiwakabidhi baadhi ya wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Afya nchini Muongozo wa Matibabu na orodha ya dawa wakati wa uzinduzi wa Muongozo huo leo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...