Timu mbili zaidi zimethibisha zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya taifa ya kuogelea kwa vijana wa umri  kuanzia miaka  saba mpaka 14 yaliyopangwa kuanza Ijumaa (Januari 26) na kumalizikia Jumamosi (Januari 27).


Timu hizo ni Mwanza Swim Club na Isamilo kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa klabu ya Dar Swim Club (DSC), Inviolata Itatiro. Klabu hizo zinaungana na Bluefins, Arusha Swim Club, Shule ya Kimataifa ya Moshi, na Champion Rise.


Vilabu vingine kwa mujibu wa Inviolata ni Taliss, Hopac, Wahoo ya Zanzibar, Kennedy House, Shule ya Kimataifa ya Morogoro na wenyeji, DSC. Inviolata alisema kuwa,  Kisima Water, Knight Support,    Coca-Cola,  Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Label Promotions, Print Galore Ltd na kituo cha televisheni cha ITV wamejitokeza kudhamini mashindano hayo.
Alisema kuwa bado wanaendelea kutafuta wadhamini ili kufanikisha mashindano hayo yenye lengo la kuendeleza mchezo wa kuogelea nchini na hasa waogeleaji chipukizi ambao ni nguzo ya nchi katika mashindano yajayo ya kimataifa.


“Maandalizi yanaendelea na kwa sasa tunaomba wadhamini watusaidie kufanikisha mashindano haya, ni mashindano ya vijana wadogo ambao wanahitaji kuona kila kitu kinakuwa sawa, ni muhimu kupata msaada kutoka kwa wadau na makampuni,” alisema Inviolata.



Alisema kuwa klabu yake inaandaa mashindano hayo kwa mara ya pili na mafanikio yameanza kuonekana kwani kuna waogeleaji wengi chipukizi wameanza kuwa tishio katika mashindano ya Taifa. Alifafanua kuwa wamepewa kibali na Chama Cha Kuogelea Nchini (TSA) kufanya mashindano hayo  ambayo awali yalikuwa ya ngazi ya vilabu kabla ya kupasishwa kuwa ya kitaifa.
waogeleaji chipukizi wakijifua

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...