NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), umejipanga vema kuendelea kutoa huduma bora kwa wadau, hususan katika kipindi hiki ambacho Mfuko unategemea ongezeko kubwa la waajiri na wafanyakazi, kutokana na mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kujenga uchumi wa viwanda, ambao utaongeza ajira.

Hayo yamesemwa leo Januari 17, 2018 mjini Morogoro na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), ili kuongeza ujuzi kwenye utekelezaji wa majukumu ya Tume.

“Katika jambo hili la kujenga uchumi wa viwanda,  makampuni mengi yataanzishwa, kutakuwa na waajiri wengi, ongezeko la wafanyakazi, kwa hivyo unategemea kwamba hitajio la utoaji huduma za Mfuko kwa wadau  litaongezeka na Mfuko umekuja wakati muafaka na tupo kwa ajili ya kuwahudumia wale wote watakaopatwa na majanga mahala pa kazi lakini pia kuelimisha.” Alisema Bw. Mshomba.

Bw. Mshomba  alisema, kuanzia Julai, 2016 Mfuko ulianza kupokea madai ya Fidia yanayotokana na kuumia au kuugua mahali pa kazi.

 Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, (kushboto), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, (wkawanza kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw.Shanes Nungu, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa Waamuzi, Wasuluhishi na Makatibu Muhtasi kutoka Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) mjini Morogoro leo Januari 17, 2018. Bw. Kalonga alimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Eric Shitindi.
Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga,kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Eric Shitindi, akifungua mafunzo hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa hotuba yake.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...