WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara ya kukagua maendeleo
ya ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na
kuagiza Wakala wa Majengo(TBA)na Suma JKT kuangalia njia bora ya kulifanya
jengo hilo liweze kukamilika kwenye ubora unaotakiwa ili watumishi wahamie.
Watumishi wa Halmashauri hiyo kwasasa wanatumia
jengo la Mkuu wa wilaya hiyo kutokana na jengo lao kutokamilika.Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kukagua
utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mwezi Novemba mwaka jana, ambapo aliagiza
ujenzi huo ukamilike ifikapo Januari mosi mwaka huu.Akizungumza wakati wa kukagua ujenzi huo, Jafo
amesema ameridhishwa na sababu zilizotolewa zilizofanya kukwama kukamilishwa
kwa jengo hilo.
“Jengo hili awali lilikuwa linajengwa na mkandarasi
mwingine lakini kutokana na utendaji wake kutoridhisha tuliamua kumpatia Suma
JKT na niliagiza jengo likamilike Januari mosi mwaka huu, lakini bado
halijakamilika,”alisema
Amesema sababu zilizotolewa ambazo mkandarasi
amekumbana nazo ameona ni vyema watumishi wakaendelea kuvumilia kutumia ofisi
ya Mkuu wa wilaya hadi hapo itakapokamilika kwenye ubora unaotakiwa.Waziri Jafo amewataka kuifanya tathmini hiyo na
kwamba kwa kuwa wanaelekea katika mipango ya bajeti wataangalia namna ya
kushirikiana na Halmashauri ili jengo liweze kukamilika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akitoa maagizo kwenye ukaguzi wa ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi jengo la Halmashauri ya Chamwino mkoani Dodoma.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...