*Polisi yaendelea kuchunguza kifo cha Akwilina,waua majambazi  Dar

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema linamshikilia mwanamke mmoja na mwanaume mmoja kwa tuhuma za kuhusishwa na mauaji ya kada wa Chadema  Daniel John  aliyekutwa amekufa maeneo ya Coco Beach jijini.

Akizungumza leo, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema kutokana na uchunguzi unaendelea kuhusu mauaji hayo huko maeneo ya Hananasifu Kinondoni wamefanikiwa kuwakamata  watu wawili.

Amesema majina ya watu hao yamehifadhiwa kwa lengo la kutoharibu uchunguzi unaoendelea kuhusu tukio hilo la mauaji ya kada huyo wa Chadema.

UCHUNGUZI KIFO CHA AKWILINA WAENDELEA

Wakati huohuo, Kamanda Mambosasa amesema bado wanaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Usafirishaji Akwilina Akwiline aliyefariki dunia baada ya kupigwa risasi.

Mambosasa amesema bado wanaendelea kuchunguza tukio hilo ambalo limegusa hisia za watu wengi na baada ya kukamilisha uchunguzi wao watatoa taarifa kwa umma ili ujue.

WAKAMATA SILAHA TANO, RISASI 35

Pia Mambosasa amesema Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa takriban wiki mbili sasa wamekuwa wakifanya operesheni ya kukamata wahalifu wanaojihusisha na matukio ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali jijini.

Amesema maeneo ya Pugu  alikamatwa mtu mmoja aitwaye Peter Kwema a.k.a Babu na alipohojiwa alikiri kujihusisha na matukio ya ujambazi katika mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Arusha,Tanga na Kilimanjaro.Pia ametaja baadhi ya wenzake ambao amekuwa akishirikiana nao.

"Baada ya kumhoji alikubali kwenda kutuonesha ambako wenzake wapo lakini baadae aliamua kupiga kelele kuwashutua kwa lengo la polisi washambuliwe ili yeye atoroke.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...