Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeipiga kalenda kesi ya Uhujumu Uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh.Bilioni 2.4,  inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini nchini,  Archard Kalugendo na mwenzake hadi Februari 27, mwaka huu.

Hatua hiyo, imekuja leo baada ya upande wa mashataka  uliokuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Estazia Wilson kuieieleza Mahakama kuwa jadala la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP)

Karugendo na mwenzeke, Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu wanakabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh.bilioni  2.4.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Godfrey  Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 27, mwaka huu itakapotajwa tena.

Inadaiwa kati ya Agosti 25 na 31, mwaka 2017  katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini  wa madini waliisababishia hasara Serikali kiasi hicho cha fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...