Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
 MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) iliendesha ukaguzi maalum wa dawa , vifaa tiba na vitendanishi katika Halmashauri na Manispa zilizo Kanda ya Kati na kubaini kuwepo kwa vifaa tiba na vitendanishi bandia duni ambavyo hajasajiliwa pamoja na dawa za serikali katika maduka ya dawa binafsi. 
 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo , Agnes Kijo amesema kuwa mamlaka haitawaacha watu wafanye vitu kiholela pamoja na kuwafikisha watuo ho mahakamani. 
 Amesema ukaguzi huo umefanyika kati ta Februari 5 hadi 7 mwaka huu katika Manispaa ya Dodoma , Morogoro na Mkoa wa Singida umefanyika katika wilaya ya Manyoni , ,iramba , Wilaya ya Gairo ,Mvomero , Kongwa na Chamwino. 
 Kijo amesema jumla ya maeneo yaliyofanyiwa ukaguzi 172ambapo 48 ni Famasi za dawa za binadamu , tano ni Famasi za dawa za mifugo ,tatu ni Hospitali na tatu zingine vituo vya afya , 76 ni maduka ya dawa muhimu za binadamu , 30 ni maduka ya dawa muhimu za mifugo, 1 ni zahanati pamoja na sita vituo vya huduma za tiba za mifugo . 
 Amesema kuwa katika ukaguzi wamepata makopo 12 ya dawa bandia aina ya Ampicillin 250mg ambapo ni tofauti na dawa halisi ya Ampicillin iliyosajiliwa na TFDA.  Amewataka ambao wenye bidhaa ambazo wanaziuza na kuweka katika mitandao wajisalimishe bila kufanya hivyo hatua kali za zitachukuliwa.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Agnes Kijo akionyesha kopo lenye dawa aina ya Ampicilin isiyosajiliwa na mamlaka hayo  jijini Dar es Salaam.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi , Mkuu  Msaidizizi wa Makosa ya  Kihalifu ya Mitandao , Joshua Mwangasa akizungumza kuhusiana na makosa ya kimtandao kwa wanaotangaza dawa  katika mitandao ya kijamii leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...