Waziri wa Nishati,  Dkt Medard Kalemani,  amefungua mafunzo ya siku Tano ya wasimamizi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) yanayohusisha wataalam kutoka Wizara ya Nishati, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) yanayolenga kuboresha utekelezaji wa mradi huo.

Mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma yamehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Michael Nyagoga, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga. 

Akifungua mafunzo hayo, Dkt Kalemani  ametoa maagizo mbalimbali ikiwemo;  wakandarasi wa umeme vijijini mara wanapomaliza kazi za usambazaji, wanapaswa kukabidhi mradi huo kwa TANESCO na REA kabla ya kuondoka katika eneo husika ili kama kuna mapungufu, yarekebishwe kabla ya makabidhiano rasmi.

Pia amewaagiza wasimamizi wa mradi huo, kuruhusu wananchi kulipia kidogo kidogo malipo ya uunganishaji wa umeme na wanapokamilisha malipo hayo waunganishiwe umeme ndani ya Siku Saba.
Vilevile ameagiza wasimamizi  wa mradi wa REA III kutoka Wizara, TANESCO na REA kuhakikisha kuwa,   wanakuwepo katika eneo la mradi ili kusimamia wakandarasi na hivyo kuongeza kasi na ufanisi katika utekelezaji.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akifungua mafunzo kwa wasimamizi wa mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) yanayofanyika katika Chuo cha Mipango jijini Dodoma.


 Wataalam wanaosimamia mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani)wakati akifungua mafunzo hayo. HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...