Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

Tanzania imeng'ara kwa nchi za Afrika kwa kuwa nchi pekee ya kwanza kuandaa kongamano linalowakutanisha wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) kutoka mataifa mbalimbali duniani. Hayo yamezungumzwa na jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Damu (Haematology), MUHAS Prof. Julie Makani wakati akielezea mafanikio ya kongamano la wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) linalokutanisha watalaam wa Tanzania na mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Bara la Afrika. 

"Nitoe pongezi kwa serikali na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya afya na ndiyo maana kila kukicha kunakuwa na mabadiliko yanayopelekea kutokea matokeo chanya, wagonjwa badala ya kukimbilia nje ya nchi wanapata matibabu ndani" amesema Prof. Makani. 

Kongamano hilo lililoandaliwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Mfuko wa Kimataifa kusaidia masuala ya elimu Menarini (Fondazione Internazionale Menarini) la nchini Italia, ambalo limeweza kuwakutanisha madaktari bingwa ikiwemo watoa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology) takribani nchi zipatazo 15 barani Afrika wanaojadili changamoto wanazokumbana wakati wa utoaji wa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology). 

Aidha Prof. Makani amesema kuwa mpaka sasa Tanzania imeweza kujitahidi kufanya jitihada za kipekee katika utoaji wa huduma japo changamoto inayowakumba ni uhaba wa wataalam zaidi wanaopenda kusomea utoaji wa huduma ya magonjwa ya damu (Haematology). 
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Damu (Haematology), MUHAS Prof. Julie Makani (kulia) akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuelezea mafanikio ya kongamano la kwanza la wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) linalokutanisha watalaam wa Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla. Pembeni yake ni Msimamizi wa Mafunzo hayo Prof. Lucio Luzzatto. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
 Msimamizi wa Mafunzo ya Wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) Prof. Lucio Luzzatto akionyesha chembe chembe zinazosababisha upungufu wa tamu mwilini wakati wakizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam. 
Wataalam wa magonjwa ya damu (Haematology) kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwemo bara la Afrika wakiwa katika sherehe ya kukaribishwa nchini Tanzania. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...