Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MEYA wa Jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita amepokea ugeni wa viongozi mbalimbali wa Jiji la
Kampala nchini Uganda wakiongozwa na Waziri wa Jiji hilo Bennie
Namugwanya Bugembe ambao wamekuja kujifunza na kupata uzoefu wa
kuendesha na kusimamia shughuli za Jiji.
Akizungumza leo jijini
Dar es Salaam Meya Mwita amesema anaamini viongozi hao kuna mambo mengi
watajifunza kwa kipindi ambacho watakuwa katika Jiji hilo huku
akiwahakikisha watapata kila wanachokitaka.
Mwita amesena kuna
mambo mengi mazuri ambayo yanefanyika na yanaendelea kufanyika katika
Jiji la Dar es Salaam hivyo viongozi hao wa Jiji la Kampala kuna mambo
watajifunza kwa ajili ya kuliboresha Jiji lao huku akiwahimiza kibuni
vyanzo vipya vya mapato ili fedha zitakazopatikana wazitumie kufanya
maendeleo.
Amesema kuwa ni vema wakatambua Jiji la Dar es Salaam
kupitia viongozi wake wa ngazi mbalimbali wamefanikiwa kutatua
changamoto mbalimbali ikiwamo ya usafiri kwa kuanzisha huduma ya usafiri
wa mabasi ya mwendo kasi pamoja na treni ya Jiji.
"Nafahamu kuna
mambo mengi ya kujifunza kutoka Jiji la Dar es Salaam,hivyo niwaombe
mtakapokuwa hapa kila ambacho mnataka kufahamu basi kuweni huru kuuliza
watalaam na viongozi wetu ambao wapo tayari kutoa majibu.
"
Tumeweka mfumo mzuri katika kukusanya kodi ni vema mkajifunza na
mtakaporudi Kampala muweke mikakati ambayo itasaidia kuwaongezea mapato
na hatimaye mtafanya maendeleo kwa ajili ya wananchi ambao
wamewachagua,"amesema Mwita.
Baadhi ya viongozi wa Jiji la Kampala nchini Uganda wakiwa kwenye ofisi za Meya wa Jiji la Dar es Salaam ambao wamekuja kujifunza namna ya kusimamia shughuli za Jiji
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita(kulia) akiwa na Waziri wa Jiji la Kampala nchini Uganda Bennie Namugwanya Bugembe ambaye yupo katika Jiji hilo kwa lengo la kujifunza na kubadilisha uzoefu wa kusimamia shughuli za Jiji
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...