Leandra Gabriel na Karama Kenyunko Blogu ya jamii
SERIKALI imesema ipo katika mpango wa kutengeneza muongozo ambao utasaidia katika utoaji huduma kwenye hospitali binafsi ikiwemo suala la ongezeko la gharama ambazo zinawafanya wananchi wa kawaida kushindwa kupata huduma.

 Mkurugenzi  wa tiba kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema hayo leo Novemba 20.2018 wakati wa uzinduzi wa mkutano wa 19 wa wadau wa afya na hospitali binafsi. Amesema kuwa muongozo huo utasaidia hospitali binafsi ambazo hutoa huduma  kwa gharama kubwa kuacha kuwabagua wagonjwa wa dharula kwani ni lazima afya ya mtu ije kwanza.

"Tunashughulikana  hospitali zenye  tozo kubwa kwa wagonjwa, kwani ni sawa kwao kuweka gharama zao kutokana na mfumo wa kutibu magonjwa maalumu, ni sawa kwa hospitali hizo kuwa na gharama zao ila kwa magonjwa ya dharura lazima huduma zitolewe bila kuangalia hadhi ya hospitali hizo" ameeleza Dkt. Gwajima.

Aidha amesema kuwa malengo ya kufanya mkutano huo ni kujadili juu ya kuimarisha utoaji wa huduma katika vituo vyao vya kutolea huduma. Dkt. Gwajima amesema kuwa sekta binafsi zinamiliki asilimia 40 za  utoaji wa huduma za afya nchini  na pia wanashiriki sana katika utoaji ajira na wao kama serikali wanatambua mchango wao na changamoto zao lazima wazifanyie kazi.

Aidha amesema kuwa  kuwa sekta binafsi ni muhimu na pasipo sekta binafsi  utoaji wa huduma za afya hazitaweza kutekelezeka kwa ubora hivyo lazima kuwepo na mabadiliko katika mtazamo chanya wa kusimamia sera za afya. Amesema kuwa bado serikali inaendeleza mikakati ya kuongeza wataalam wa afya katika vyuo mbalimbali ili kuongeza huduma bora katika vituo vya afya nchini.
 Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa vituo vya afya binafsi nchini (APHFTA) Dkt. Kaushik Ramaiya (kushoto) akifuatilia mjadala uliozinduliwa na Mkurugenzi wa tiba kutoka Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima(kulia) leo jijini Dar es Salaam, wa pili kutoka kulia ni Afisa mtendaji wa APHFTA Dkt. Samwel Ogillo. (Picha na Erick Picson, Blogu ya jamii)
Mkurugenzi wa tiba kutoka Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati akifungua mkutano wa 19 wa wanachama na wamiliki binafsi wa vituo vya afya leo jijini Dar es Salaam.
 Afisa mtendaji  wa wanachama wa wamiliki binafsi wa vituo vya afya Dkt. Samwel Ogillo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo ambao umejikita zaidi katika kujadili namna ya kuimarisha zaidi sekta ya afya nchini .
Afisa mtendaji  wa wanachama wa wamiliki wa vituobinafsi vya afya Dkt. Samwel Ogillo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo ambao umejikita zaidi katika kujadili namna ya kuimarisha zaidi sekta ya afya nchini .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...