Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akiangalia baadhi ya vifaa vinavyotengenezwa na Kampuni ya Uzalishaji wa fenicha na Uuzaji wa mashine ya Azienda Group Limited, katika banda la wajasiriamali wadogo na wa kati lililodhaminiwa na benki ya NBC wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba hivi karibuni. NBC mdhanini mkuu wa maonesho hayo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara za Kibenki, ElvisNdunguru na kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Kibiashara wa Azienda Group Limited, Hekala Sigalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto), akitembelea banda la wajasiriamali lililodhaminiwa na Benki ya NBC wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba hivi karibuni. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi. NBC ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo.
Ofisa Mahusiano wa Benki ya NBC, Lena Mwakisale (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya watu waliofika katika banda la Kliniki ya biashara lililodhaminiwa na benki hiyo wakati wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba jana. Kulia kwake ni baadhi ya wafanyakazi wenzake. NBC ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo.
Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Upendo Njogolo (kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na NBC na pia katika banda la benki hiyo wakati wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba, jijini humo jana. NBC ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo.
Ofisa Mkuu wa Usimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Justine Katiti (kulia) akizumzumza na Mfanyabiashara Saidi Lugendo, kuhusu masuala ya kodi katika banda la Kliniki ya biashara linalodhaminiwa na benki ya NBC wakati wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana. NBC ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
Mshauri wa Mambo ya Kibiashara wa Kampuni ya Uzalishaji wa fenicha na Uuzaji wa mashine ya Azienda Group Limited, Hekala Sigalla (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), kuhusu vifaa vinavyotengenezwa na kampuni yake katika banda la wajasiriamali wadogo na wa kati lililodhaminiwa na benki ya NBC wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba hivi karibuni. NBC mdhamini mkuu wa maonesho hayo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara za Kibenki, Elvis Ndunguru.
Baadhi ya watu wanaofika katika maonesho ya Sabasaba wakipata taarifa mbalimbali kuhusu huduma za kibenki za NBC pamoja na masuala mengine ya kibiashara kutoka kwa washirikika wa NBC kama vile TRA, BRELA, TBS na wengineo katika katika banda la Kliniki ya Biashara ya NBC lililodhaminiwa na benki hiyo.
Benki
ya Taifa ya Bishara kwa mara nyingine tena imekuwa mdhamini wa maonesho ya 44
ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika Kurasini jijini
Dar es Salaam katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere kuanzia Julai
1 hadi 13 mwaka huu.
Maonesho
hayo ambayo yanakutanisha wajasiliamari, Wafanyabiashara, Wazalishaji na Watoa
huduma mbalimbali yanafanyika katika kipindi ambacho wananchi wanatakiwa
kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mapafu maarufu kama Corona.
Theobald
Sabi, Mkurugenzi Mtendaji NBC katika uzinduzi wa maoneesho hayo leo, amewaambia
Waandishi wa Habari kuwa lengo kuu la udha mini wa benki hiyo kwa taasisi hizo
za fedha ni kuwawezesha wajasiliamari wadogo na wa kati ambao ndiyo walengwa
wakuu wa maonesho hayo kujifunza na kutumia fursa zilizopo katika soko la ndani
la nje katika kuuza bidhaa na huduma wanazozizalisha na kuzitoa.
Benki
ya NBC pia inalenga katika kuwasogezea wateja wake huduma zake karibu zaidi
kupitia maonesho hayo.
“Katika
benki yetu ya NBC tunayo huduma maalumu ambayo inalenga katika kuwawezesha
wajasiliamari, wafanyabiashara wadogo na wa kati kuona na kuchangamikia fursa
za masoko ya ndani nay a nje ya bidhaa na huduma wanazozitoa na kuzalisha;
Pia
tumekuwa tukitoa mafunzo ya kibishara kwa makundi haya ya wafanyabiashara,
kuwafundisha mbinu za uzalishaji bora na ufungashaji wa bidhaa zao ili ziweze
kuvutia na kushindana kimataifa” alisema Sabi.
Elvis
Ndunguru, Mkurugenzi wa Huduma za Biashara za Kibenki kutoka NBC Alisema kuwa
benki ya NBC imewaalika wajasiriamali wadogo na wa kati ambao ni wanufaika wa
mafunzo na uwezeshwaji wa NBC.
Aliwataja
wajasiliamari hao kuwa ni Miku Investment Company Limited wazalishaji na wauzaji
wa vipodozi, Borah Lemmy Rothblets wauzaji wa asali na mafuta ya
alizeti,Takecharge International Limited, na Azienda Group Limited wazalishaji
wa samani na mashine. Wengine ni kampuni za Chelsea Tyre Tube wauzaji wa vipuri
vya magari na kampuni ya Dagen Traders wauzaji wa vitenge.
“Baadhi
ya wajasiliamari hao wamealikwa na benki katika maonesho ya biahsra ya mwaka
huu watatumia fursa hiyo kudhihirisha ni kwa namna gani NBC imekuwa taasisi
muhimu katika kuwawezesha na hivyo kuchangia ukuaji wao. Tumekuwa pia
tukiwawezesha wajasiliamari katika sekta ya madini, ufugaji kuku, ng’ombe,
mbuzi, sekta ya uzalishaji amzao ya kilimo na uvuvi” aliongeza Ndunguru.
Akifungua
maonesho hayo Ijumaa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezisifu beni za biashara
nchini kwa mchango wake wa kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati kabla ya
mwaka 2025. Alisema sekta ya fedha ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa
mwananchi mmoja mmoja na hatimaye taifa kwa ujumla.
“Serikali
itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi zikiwemo benki za
biashara ili ziendelee kufanya kazi zake vizuri na kwa mafanikio. Serikali
inazihimiza benki kuendelea kuto amikopo ya masharti na riba nafuu kwa
wafanyabiashara hususani wajasiriamali ili waweze kukuza biashara zao na hivyo
kuongeza wigo wa vipato vyao na ajira” alisema Majaliwa.
Kampuni
ya Chelsea Tyre Tube inayojishughulisha na uingizaji na uuzaji wa vipuri vya
magari na m,atairi imekuwa mnufaika wa mikopo ya NBC tangu mwaka 2004 na
inajivunia ukaribu wake na NBC katika mafanikio ya bishara yake.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni hiyo Martin Massawe, alisema kuwa kampuni yake imekuwa
mnufaika wa mikopo ya masharti na riba nafuu kwa miaka zaid ya kumi hivi sasa.
Alisema kuwa kampuni imekuwa na mtandao mzuri wa kibiashara kutokana na
ushirika wake na NBC. Pia mafunzo mbalimbali yametolewa kwa wafanyakazi wa
kampuni yake juu ya kujenga mahusiano ya kibiashara na utafutaji soko.
NBC
ni benki yenye uzoefu zaidi nchini ambayo imekuwa ikitoa huduma za kifedha kwa
miongo mitano sasa ikihudumia wateja binafsi, biashara ndogo, kubwa, makampuni
na uwekezaji. Kwasasa benki ina mtandao wa mawakala zaidi ya 3,000 wakitoa
huduma katika matawi yake 49 yaliyosambaa kote nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...