Watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) wametakiwa kusimamia Sheria za Uhifadhi ili kunusuru maisha ya Wanyamapori ambao wamekuwa wakidhuriwa na Wananchi wanaovamia Mapori ya Akiba na Hifadhi kwa kufanya ujangili.

Agizo hilo limekuja kufuatia kuwepo kwa wimbi la Wananchi kuvamia hifadhi  na kuua Wanyamapori huku wakipata utetezi toka kwa baadhi ya Wanasiasa.

 Hayo yamesemwa na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA  Mej.Gen(Mstaafu) Hamisi Semfuko katika hafla ya kufunga mafunzo ya Kijeshi kwa watumishi 150 wa TAWA ikiwa ni utekelezaji wa mabadiliko ya utendaji kazi kutoka mfumo wa Kiraia kwenda wa mfumo wa Kijeshi.Mafunzo hayo yalifanyika eneo la Fort Ikoma katika wilaya ya Serengeti 22/12/2020.
Kwa upande wake Kamishna wa Uhifadhi kutoka TAWA Bw.Mabula Misungwi alitoa shukrani nyingi Kwa Uongozi wa wilaya ya Serengeti na wadau wa Uhifadhi katika kuonyesha mshikamano wa dhati kuunga TAWA katika kupambana na ujangili.

Aidha.Bw.Mabula aliwataka wahitimu wakatumie ujuzi waliopata katika mafunzo hayo kuwa wazalendo nĂ¡ kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Bw.Nurdin Babu amesema yupo tayari kushirikiana na TAWA katika kuhakikisha wananchi hawavamii maaeneo yaliotengwa kwaajili ya  hifadhi.
"Sasa kazi ni moja tu, kupambana na changamoto dhidi ya Wananchi wanaovamia Mapori ya Akiba na Hifadhi za Taifa”

Mafunzo haya ya jeshi usu ni ya 11 kwa TAWA tangu mfumo wa kijeshi uanzishwe . Mfumo huu wa kijeshi umeleta mabadiliko makubwa kwa Watumishi tangu kuanzishwa kwake  ambao umebeba picha ya Uzalendo.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...