Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Raisi wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt Tulia Ackson amaetoa Rai kwa Waandishi wa habari na Watangazaji Nchini kutumia muda wao kuandika na kuhabarisha Umma kuhusiana na Mazingira pamoja na Mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Dkt Tulia ameyasema hayo mapema Leo hii May 2 Jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la wana habari kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambayo hufanyika May 3 kila mwaka.

"Nitoe Rai kwa Waandishi wa habari na Watangazaji kutumia muda wenu kuandika habari za kuhabarisha Umma kuhusiana na mazingira na mabadiliko ya tabia ya Nchi,hasa katika kipindi ambacho tunakipitia ambacho wakati mwingine sio mara zote watu huusisha na kila jambo linalotokea katika jamii ili mradi nila mazingira basi tunalihusisha na mabadiliko ya tabia ya nchi,Tunawategemea sana katika kuhabarisha na kuelimisha Umma kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi ".

Aidha Dkt Tulia amesema kuwa takwimu za Watafiti zinaonesha kuwa takribani watu milioni 16 nchini Tanzania wanategemea rasilimali za pwani kwaajili ya kuendesha maisha yao hivyo uharibifu ukitokea unaathiri hao watu wote milioni 16 hivyo wasimame hapo kuokoa mazingira pia".

"Takwimu za watafiti zinaonesha kuwa takribani watu milioni 16 nchini Tanzania wanategemea rasilimali za pwani kwaajili ya kuendesha maisha yao,na kwahiyo uharibifu wote unaotokea unahatarisha maisha ya hao watu milioni 16, Katika Muktatha huo tunawagemea Waandishi wa habari kusaidia kuokoa haya mazingira ambayo na ninyi kwa kuona umuhimu wake tunaamjni mtafanya uchunguzi lakini pia ninyi mmeweka kwenye kauli mbiu yenu kuonesha kwamba mtashiriki pamoja na sisi kwenye jambo hilo".

Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi, Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe Nape Nnauye yeye amesema kuwa kazi ya vyombo vya habari hapa Nchini ni nzuri hata kama hatujafika tunakokutaka lakini tumepiga hatua sana katika sekta hii.

"Kwa kifupi niseme kazi ya ya vyombo vya habari ni nzuri hapa Nchini kama nilivyotangulia kusema, inawezekana hatujafika tunakotaka kwenda lakini tumepiga hatua kubwa na tunaendelea kusonga mbele na Serikali ya awamu ya 6 chini ya usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameruambia tuache milango wazi kila tunapohitajika na kila panapohitajika kufanya marekebisho ya hapa na pale".

Kongamano hili limehudhuriwa na wadau wa Sekta ya Habari Nchini wapatao 300 wakiongozwa na Kauli mbiu isemayo:Uandishi wa habari katikati ya Changamoto za Mazingira.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...