waandamanaji leo manzese

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Wazee mliyeko bongo kweli hili swala Rada linashughulikiwa au?Unajua Serkali ilikua haina pesa cash za kununua huo mtambo hivyo imechukua mkopo na bado tunalipa riba ya huo mkopo mpaka saa hii riba yenyewe ni 3Percent piga hesabu babaake tangia hizo siku za mzee Beni na babaako Fedrecki Sumaye mpaka leo na kesho na kesho kutwa huo mkopo wazungu wao wanakula riba tu,umasikini tutaukwepa kwa jinsi hii jamani?
    Mlarushwa,UK.

    ReplyDelete
  2. Naona Wadanganyika pole pole wanaanza kuamka ...Haiwezekani watu wachache watufanye sisi wajinga ! Kulikuwa hakuna sababu yoyote ya kununua hiyo rada at the first place zaidi ya kamisheni .

    ReplyDelete
  3. bora wangekaa kimya tu,kwani kulikuwa na muda wa kutosha kufanya haya maandamano, hapa naona ni kama kudandia gari kwa mbele

    ReplyDelete
  4. Mimi sio pilitician na wala sipendi mapolitician period. Lakini kabla hatujaanza kulumbana kwanza tuangalie pande zote mbili.

    1st kwanini Uingereza iwe na hamu ya kuchunguza kuwa "why we bought a rada?" ni kwa vile nchi yetu ni maskini sana na hatuna hiyo hela au wanaona uchungu sana hiyo hela tungeitumia kwa manufaa mengine ya sisi masikini? au wanajua nchi yetu ni maskini sana hivyo hiyo hela hatuna na tumepewa na nani??
    2nd labda hiyo rada ukiangalia kwa wakati tunaoishi mambo ya materrorist labda hoyo rada no so powerful na hata hatutaitumia kwa mambo yetu ila itatumiwa na watu wa nchi nyingine kupitia kwetu
    3rd sisi nchi yetyu ni masikini na tuna uarafiki na nchi za kiarabu ...mwingereza anataka kujua kukweli isije kwesho hao waarabu wakatututmia sisi kuwavamia.
    4th kwanini rais aondoke aende uingereza halafu mara uarabuni...???

    Kama kuna walio nufaika na hiyo biashara ni wachache lakini hii rada itatuletea majanga kwa nchi yetu yote hapo baadaye. Inaweza kutusaidia kulinda lakini at this time serious do we need a rada to protect ourselves?? We hardly eat....before someone comes to attack us we will be all starve dead...

    ReplyDelete
  5. Watoa maoni hapo juu,

    Kwanza riba ni 4.9% na tunawalipa Barclays bank.

    Pili suala la UK kuchunguza sio kwasababu wanataka kutusaidia sisi, bali ni kwasababu wanataka kukomesha rushwa kwenye nchi yao kama sheria zao zinavyodai. Uchunguzi huo pia unahusisha
    Saudi Arabia na South Africa.

    Hayo ya kuwa na uhusiano na Waarabu, nafikiri TZ tuna haki na uhuru wa kushirikiana na nchi yoyote. Hatuchaguliwi marafiki au maadui.

    Kuhusu rada kwa ujumla tumefungwa magoli na wajanja wachache wakishirikiana na wageni wanaojiita Watanzania. Ukiwapekua utakuta wana passport za UK

    ReplyDelete
  6. Anon wa hapo juu amesema point mpaka pale alipoongelea suala la pasport za UK .What is wrong with that !
    Kwa taarifa yako wao ni wadosi na appart from passport za UK labda wana za India pia ! Big deal ?
    Usiniambie kama wewe ni mzalendo kiasi kwamba kwasababu hujawahi kusafiri ungekataa $12m za wadanganyika !
    Any way Sheria ichukue mkondo wake

    ReplyDelete
  7. manzese kumekuwa kusafi!

    ReplyDelete
  8. MY DEAR TANZANIAN
    Imefika wakati kufumbua macho tumedanganywa vya kutosha tangu uhuru.. Tanzania inanunua rada ya kazi gani sie hatuna maadui wa kutoka nje. ila maadui wetu ni umasikini na magonjwa...hiyo rada imenunuliwa ili kumwangalia nini??? serikali baada ya kufikilia kujenga hospitali yenye hadhi ya hospitali kuu -Dar-es-salaam wanafumba macho na kulizika na Muhimbili kajengo ambako kana adhi ya wilaya , kitu cha kushangaza ni kwamba hata basi hiyo Muhimbili haina vitanda vya kutosha watu wana lala watatu kwenye kitanda.. aibu iliyoje??/ leo mnanunua rada hao wazungu wanao tupa hizo hela wanabaki kushangaa kwasababu nilisoma kwenye New york times kuhusu hiyo rada wanakuambia kwanza Africa mzima hakuna halafu katika G8 ni nchi tatu tuu zenye rada kama hiyo hiyo inatosha kukaa chini na kutafakari .how much it cost????Tanzania ina majukumu mengi yanayo hathiri almost 90 per cent of all population watu wanaenda kununua rada... Jiji kuu hakuna maji Dar ,hakuna umeme nilikuwa huko last summer city centre uwezi kuongea na simu generator zinavyo unguruma, uchafu kila sehemu picha ya Michuzi -(Bafu )hayo ndiyo maisha ya wakazi wa jijini asilimia kubwa ....serikali inafumba macho na kununua rada ya billion of dollars ambazo tuna pewa na wazungu tujenge shule ,hospitali,maji ,umeme na vitu MUHIMU kwa watanzania(majority siyo minority) lazima watu wawajibike kuhusu hii issue vinginevyo kasi mpya na mambo mapya tutaanza kuyatilia wasiwasi.
    Doctor///

    ReplyDelete
  9. Mwanangu Michuzi hebu niwekee hii article niliyoichukua toka gazeti la mwananchi. Tafadhali usiniweke kapuni. Sasa yuko wapi? Basil wa Mramba aliyedai kwamba hata majani tutakula lakini Rada lazima inunuliwe. Alikuwa mstari wa mbele kupiga debe la ununuzi wa rada hiyo, sasa kuna mnuko wa rushwa mbona kaingia mitini?

    Maswali ya kujiuliza kwa nini hawa wahindi bado wanatesa uraiani wakati kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani? Nani anawakingia kifua? Mkapa naye mbona amepata kigugumizi na aliwahi kudai kuna rushwa ndogo ndogo tu, ha nii nayo ni ndogo? Hawa wahindi walijuaje kama kuna zabuni ya kununua ndege na rada? zilitangazwa na Ikulu, wizara ya fedha au wizara ya usafirishaji? Zilitangazwa lini na katika gazeti gani la Tanzania?

    Kikwete ashughulikie bomu hili kwa kuwatia ndani hao wadosi na waminywe ili waseme katika mgao huo nani walihusika, pia watoe permission ili transactions zote zilizofanyika katika bank accounts zao tangu zilipoingia hizo $12 millions hadi leo zichunguzwe kwa kina.
    ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

    Wapinzani wataka ufisadi, rada, mikataba,vichunguzwe

    Muhibu Said na Patricia Kamelemeta
    VYAMA vitano vya upinzani, jana vilihitimisha maandamano ya kupinga madai ya ufisadi nchini kwa kutaka iundwe tume huru itakayochunguza namna dola za Marekani milioni 12 zilivyolipwa kwa wakala aliyehusika na ununuzi wa rada ya mabilioni ya shilingi.
    Mbali na hilo, vyama hivyo vya upinzani vimependekeza tume hiyo kuchunguza vigogo waliohusika katika sakata hilo na kuwachukulia hatua iwapo watathibitika kuhusika na suala hilo pamoja na kuipitia mikataba yote yenye harufu ya rushwa.

    Akihutubia mkutano wa hadhara mara baada ya maandamano hayo katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuundwa kwa tume hiyo kutasaidia kuwarejeshea wananchi imani kwa serikali dhidi ya wasiwasi wa kuwepo kwa rushwa katika ununuzi wa rada hiyo.

    "Ufisadi unatisha. Ahadi ya tano ya TANU ilisema: Rushwa ni adui wa haki, sitatoa wala sitapokea rushwa...Tunahitaji tume huru ya watu walio safi iundwe, waweze kupitia mikataba inayonuka rushwa, waeleze hizo fedha zimeibwa wapi, nani aliyehusika na wachukuliwe hatua," alisema Profesa Lipumba na kuongeza: "Tunahitaji fedha hizo zirejeshwe mara moja".

    Alipendekeza Mhadhiri wa zamani wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Issa Shivji kuwa miongoni mwa watu wanaostahili kuunda tume hiyo akisema kwamba ni mtu safi anayeweza kufanya kazi hiyo kwa uadilifu na uaminifu wa hali ya juu.
    Profesa Lipumba alisema anashangaa kuona hadi sasa Serikali inapata kigugumizi kwa kushindwa kumkamata wakala aliyehusika na ununuzi wa rada hiyo wakati baadhi ya vyombo vya habari vya Uingereza vimekwisha kusaidia kutaja jina lake halisi, umri na mahali ziliko ofisi za mtu huyo hapa nchini.
    "Ilipaswa huyu bwana awe amekamatwa, anaisaidia polisi, Takuru (Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini), aeleze alishirikiana na wakubwa gani," alisema Profesa Lipumba na kuongeza:

    Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP), John Cheyo, aliwataka Watanzania kuchukizwa na kitendo cha matumizi mabaya ya fedha za ununuzi wa rada hiyo na kuonya kuwa iwapo ufisadi na rushwa vitaendelea, nchi itaendelea kuwa maskini, tegemezi na kuwakamua wananchi kwa kuwatoza michango isiyokwisha.
    "Ukiona mtu anachukua fedha zetu, kasirika na uchukue hatua mara moja," alisema Cheyo na kuongeza: "Tukiendelea na hali ya ufisadi na rushwa, nchi itaendelea kuwa maskini, tegemezi na changia changia".
    Mbunge wa Jimbo wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, alishutumua kitendo hicho ambacho alidai kinaonesha ni kwa jinsi gani nchi inavyotawaliwa, kuongozwa na rasilimali za nchi kutumika vibaya.
    Alisema anashangaa kuona serikali inadiriki kutumia Sh80 bilioni kununua majengo ya Quality Group Limited huku ikijidhalilisha kwa kuiomba Jumuiya ya Kimataifa msaada wa Sh 83 bilioni.
    "Tangu mwaka 2004, nchini kumekuwa na matumizi mabaya ya fedha za umma, mwaka jana vyombo vya habari viliripoti suala hilo, lakini serikali imeshindwa kuchukua hatua," alisema Kabwe.
    Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Juma Hamad Rashid, aliwataka wananchi kutoishia kutoa taarifa za rushwa Serikalini na kuwataka kufanya hivyo pia kwa vyama vya upinzani ili taarifa hizo ziweze kufikishwa bungeni, kuwapo uwajibikaji na umma na dunia waweze kuelewa.

    Naye Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema wapinzani watahamasisha kuonyesha Watanzania upungufu uliomo ndani ya muswada wa sheria ya vyombo vya habari na akawataka waungane kuupinga muswada huo.
    Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party, Augustine Mrema Alisema anamuonea huruma Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo kutokana na kauli yake ya kuwatuhumu wabunge kwa ulaji rushwa kwa kuwa yanaweza yakamkuta mabaya.

    Licha ya kuandaliwa na vyama vitano vikuu vya upinzani, maandamano hayo yaliyoanzia katika makutano ya Barabara za Morogoro na Mandela yalihudhuriwa na watu wachache kinyume na ilivyotarajiwa.
    Pia Ndesamburo ambaye awali aliahidi kuhudhuria na kueleza kwa undani sakata lake la kuwahusisha na rushwa wajumbe wa kamati ya haki, maadili na madaraka ya bunge, hakuweza kutokea na hakukuwa na taarifa zozote juu ya kutokuwapo kwake.
    Mkutano huo pia uliambatana na mgawo wa pilau na maji, vilivyoandaliwa na kamati ya maandalizi ya maandamano kwa waliohudhuria.

    ReplyDelete
  10. Watanzania tunapenda kudandia magari, hii issue ya rada iliibuliwa UK wakati huo na watu hasa wanasiasa wakajifanya kuiponda serikali utafikiri wao ndio walishtukia hilo deal. Na leo ni hayo hayo, UK wanajifanyia uchunguzi wao kama kuna rushwa ktk uuzaji wa rada, wabongo nao wanalivalia njuga suala hilo. Toka rada inanunuliwa mpaka leo tulikuwa wapi kusema? UK bado hata hawakamilisha uchunguzi na kutoa ripoti kama kuna rushwa au la, wabongo tumeshatoa majibu kwamba 10% walizopewa viongozi zipo Uswizi, mweeeee!

    ReplyDelete
  11. Mtoa maonI Anonymous

    Tanzania is a poor country, but in the past it has been the most honest in Africa. It is outrageous to learn that it has been corrupted with the connivance of UK government officials, which professes benevolence towards Africa but uses it as a dump for the surplus products of the British arms industry.

    Ministers during Mkapa's time must have known that this deal was corrupt. No sane government of a poor country would pay at least three times over the odds for unneeded equipment, against the advice of the World Bank, unless someone was taking a cut. Yet they allowed themselves to be bullied of "kitu kidogo" If BAE could sell its products by legitimate means, that was just too bad to Tanzania.
    I am so sorry to President Kikwete! HE HAS TO BITE EVEN IF HE WILL BE UNPOPULAR AMONG HIS CIRCLES.
    PRESIDENT, DO SOMETHING WE HAVE THE NAMES OF THOSE WHO GOT KITU KIDOGO. IF YOU WONT DEAL WITH THEM PUBLICLY, THEN THROUGH THIS MTANDAO WE WILL EXPOSE THEM! WE HAVE THE ACCOUNTS, NAMES, DATE OF BIRTH AND ADDRESS AND THE WAY KITU KIDOGO WAS DIVIDED.
    DO NOT UNDERESTIMATE WATANZANIA WENYE MOYO WA KUSAIDIA MAMBO YAENDE SAWA HAPO NYUMBANI.
    THANKS.

    ReplyDelete
  12. Vyama vya upinzania vikiambia vitangaze sera vinapata kigugumizi. wakisikia issue tu ya serikali ndio hapo wanapopata pa kuegemea.

    kuna mambo mengi hayaendi sawa ktk hii nchi, lakini hivi vyama hukaa kimya hadi magazeti yakishaandika na wakiona wananchi wanapinga issue hiyo nao hapo ndio wanakurupuka na kuifanya hiyo issue kuwa agenda yao na kuiteka.

    huu ni utoto na vyama vya upinzania ni lazima vibadilike ili viondokane na fikra hizi finyu.

    tunata political parties ambazo ni Pro-active na sio re-active.
    hii ni kwenu nyote CUF,CHADEMA, TLP,NCCR-Mageuzi. wengine muwapelekee meseji hii...

    issue ya rada imekuwepo toka siku nyingi. imegusiwa kidogo na facts kutolewa nao ndio wamepata pumzi na kuanza kusikika. viongozi wengine wa upinza wapo ICU kisiasa.

    ReplyDelete
  13. Mtoa maoni mwenye majina ya hao wala rushwa. Tafadhali ninakuomba tumwagie hadharani hao mbwa wanaotufanya sisi wajinga. Hakuna siri hapa mtandaoni. We want to put pressure on them, that they can return tax payer's money.

    ReplyDelete
  14. Ndugu
    mimi ninakubaliana kabisa na huyu mtanzania ambaye ana moyo au amefanya kazi kubwa ya kuchunguza hawa waliopata mgao. Huu ni mtihani mkubwa sana kwa bwana Jakaya Halfan Mrisho Kikwete na Lowaza.
    Ninasubiri tu niangalie atakapokwenda France mwezi ujao kwenye mkutano wa mambo ya kuzuia rushwa nk. SASA itakapoonekana naye anashindwa kuchukua hatua muafaka, BASI nitaweka bayana majina na formular iliyotumika kugawa mgao, kuanzia ununuzi wa ndege ya Rais ambayo na issue ya Rada
    Elimu aliyotupa baba wa Taifa nilazima tuitumie kwa kuwaelimisha watanzania ambao haki na kodi zao zinatumiwa vibaya na hawa wachache!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...