THANK YOU

In Loving Memory of Anastazia Rupia.


Dear Friends,

My family and I would like to express our sincere gratitude to you all for being there for us at the saddest moment of our lives as we lost our dear and beloved mother Anastazia Rupia. You have been and still are comforting and supporting us in many ways as we are going through this difficult bereavement period.

We would like to especially thank you for the financial assistance, your monetary contributions enabled us to meet the costs of transporting our beloved mother to Tanzania. Our dear mother Anastazia Rupia was laid to rest on Sunday January 7th, 2007.

Thank you all for your contributions, Love, Comfort and Support.

Thank you so much and May God Bless You.


Sincerely,

Stella Rupia and Family.


----------------------------------------------------------------------------------
SHUKRANI

Kumbukumbu ya mpendwa Anastazia Rupia


Wapendwa Ndugu, Jamaa, na Marafiki,

Kwa niaba ya familia yangu napenda kutoa shukrani za dhati kwenu nyote kwa upendo mliotuonyesha na mema yote mliyotutendea baada ya kupata msiba wa kuondokewa na mama yetu mpenzi Anastazia Rupia.
Tunashukuru kwa faraja mlizotupa, upendo na ushirikiano mliotupa katika kipindi hichi kigumu cha msiba wa mama yetu mpendwa. Ahsanteni sana kwa misaada ya khali na mali, hasa michango yenu ambayo imetusaidia katika kuweza kulipia gharama za usafiri kwenda Tanzania kwa mazishi.
Mama yetu mpenzi Anastazia Rupia amezikwa tarehe 7 Januari 2007 kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar-es-Salaam. Tunashukuru sana kwa yote na tunaomba Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki.

Ahsanteni sana.

Stella Rupia na familia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Poleni wafiwa na Mungu awape moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu. samahani sana Michuzi na wanablog naomba mnifahamishe kwa kuwa siifahamu vizuri hii familia, huyu aliyekuwa kwenye hii picha ndiye marehemu mama Anastazia Rupia au ni mtoto anayetoa shukurani Stellah Rupia?

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wafiwa. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana lihimidiwe. Mungu awape mioyo ya uvumilivu katika kipindi hiki kigumu mlichoondokewa na mpendwa wenu. Kimbilio letu ni Mungu, hivyo basi hamna budi kumkumbuka mama kwenye sala zenu za kila siku.Poleni sana ndugu zangu.

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  4. Anafanana sana na miriam makeba,poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete
  5. Michuzi kama kweli unachuja maoni nafikiri hayo ya huyo aliyejiita John Riwa (nafikiri ni jina bandia) usingeyatoa kwenye blog hii ya watu waliostaarabika. Napendekeza uyaondoe!

    ReplyDelete
  6. Watu kama John Riwa wamesababisha wapenzi wengine wa blog hii kuachia ngazi.

    ReplyDelete
  7. John Riwa's comment is distasteful and offensive. Please MICHUZI REMOVE it. Although I do not know the deceased family but I still cannot stand these off-the-cuff remarks.

    Heshima ni kitu cha bure.

    ReplyDelete
  8. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...